Habari za Punde

SERENGETI BOYS WAPAA JIONI HII KUELEKEA KOREA YA KUSINI

 Wachezaji wa Timu ya Serengeti Boys wakiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tayari kwa safari kuelekea nchini Korea ya Kusini kushiriki mashindano maalumu ya vijana walio chini ya umri wa miaka 17.
Wachezaji wa Timu ya Serengeti Boys, wakiwa katika foleni ya kuingia kwenye eneo la ukaguzi la uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wakati wakisafiri kuelekea nchini Korea ya Kusini kushiriki mashindano maalumu ya vijana walio katika chini ya umri wa miaka 17.
Afisa Habari wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, Alfred Lucas, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati timu ya vijana  walio chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys yenye jumla ya msafara wa watu 25 ikiondoka nchini leo kuelekea nchini Korea ya Kusini kushiriki mashindano maalumu ya vijana walio katika umri huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.