Habari za Punde

SERIKALI KUTENGA DOLLA MILLION 115 KUBORESHA LISHE NCHINI

 Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akizungumza na waandishi wa habari wadau wa harakati za upatikanaji wa lishe bora nchini  na wahariri wa vyombo vya habari katika hafla ya kuwatunuku tuzo waandishi bora wa masuala ya lishe nchini iliyofanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 22,2016.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Lishe Tanzania(PANITA) Bw. Tumaini Mkindo akielezea mikakati na utekelezaji wa mipango ya Jukwaa la Lishe Tanzania katika kuboresha upatikanaji wa lishe bora nchini katika hafla ya kuwatunuku tuzo waandishi bora wa masuala ya lishe nchini iliyofanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 22,2016.
 Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania Bw. Neville Meena akizungumza katika hafla ya kuwatunuku tuzo waandishi bora wa masuala ya lishe nchini iliyofanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 22,2016
 Mwakilishi wa Ubalozi wa Ireland na Irish Aid Bi. Neema Shosho akizungumza kwa niaba ya ubalozi kuhusu masuala ya lishe katika hafla ya kuwatunuku tuzo waandishi bora wa masuala ya lishe nchini iliyofanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 22,2016. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

   Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la  Lishe Tanzania(PANITA) Bw. Tumaini Mkindo wakati wa hafla kuwatunuku tuzo waandishi bora wa masuala ya lishe nchini iliyofanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 22,2016. 
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akikabidhi cheti zawadi ya tablet na Shillingi million 1.5 kwa Bi Tumaini Msoyowa mshindi wa kwanza wa Shindano la mwandishi bora wa habari zinazohusu lishe kutoka gazeti la Mwananchi katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 22,2016.
 Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akikabidhi cheti zawadi ya tablet na Shillingi million 1. Kwa mwakilishi wa  Bi Winny Itaeli wa mshindi wa pili wa Shindano la mwandishi bora wa habari zinazohusu lishe kutoka gazeti la The Guardian katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 22,2016.
 Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akikabidhi cheti na Shillingi laki 5 kwa Bw. Gerald Kitabu mshindi wa tatu wa Shindano la mwandishi bora wa habari zinazohusu lishe katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 22,2016.
 Washiriki wa shindano la mwaandishi bora wa habari za masuala ya  lishe pamoja na wageni waalikwa wakifuatilia hotuba mbalimbali ikiwemo ya Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura wakati wa hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 22,2016.
 Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Jukwaa la Lishe Tanzania, wahariri  wa vyombo vya habari,waandishi wa habari washiriki na washindi wa  Shindano la mwandishi bora wa habari zinazohusu lishe katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 22,2016. Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM.
**************************************************
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Serikali imeahidi kutenga jumla ya Dola za kimarekani Millioni 115 kwa ajili ya kuboresha lishe ikiwa ni  mpango wa maendeleo wa miaka mitano 2016/2021 na mkakati wa kuboresha lishe kwa mwaka 2016/2021.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipokuwa akizungumza katika halfa ya kuwatunuku tuzo waandishi bora wa habari zinazohusu lishe iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Anastazia Wambura ameongeza kuwa bado kumekuwa na changamoto katika upatikanaji wa lishe bora nchini ikiwemo kuwepo kwa tamaduni mbalimbali zinazonyima fursa kwa watoto na wakina mama kupata lishe iliyo bora.

“Serikali imeingiza suala la lishe katika mpango wa maendeleo wa taifa wa miaka mitano na katika kulitekeleza hili Serikali ya awamu ya Tano itatenga dola million 115 kwa ajili ya mkakati wa kuboresha lishe nchini” alisisitiza Mhe. Anastazia.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Lishe Tanzania(PANITA) Bw. Tumaini Mkindo amesema kuwa hali ya lishe imeendelea kuimarika hasa kwa miaka mitano iliyopita hili linadhihilisha kuwa mikakati thabiti iliyopo imesaidia kwa asilimia kubwa kupambana na tatizo la ukosefu wa lishe bora nchini.

Bw. Mkindo ameipongeza Serikali kwa juhudu inazozichukua katika kupanga mikakati na kuitekeleza katika suala la upatikanaji wa lishe bora nchini ili kuondokana na suala la  udumavu linaloleta athari kubwa katika ukuaji wa Binadamu.

Ameongeza kuwa Jukwaa la Lishe Tanzania litaendelea kushirikiana na Serikali na wadau wengine katika harakati za upatikanaji wa lishe bora na kufikia malengo ya Shirika la Afya Dunia (WHO) yaliyosainiwa na Tanzania yahusuyo masuala ya lishe pamoja na kupunguza udumavu kwa asilimia 40 ifikapo mwaka 2025

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.