Habari za Punde

*SERIKALI YAWAAGIZA WAKUU WA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI KUTOA ADHABU STAHIKI KWA WANAFUNZI WATOVU WA NIDHAMU

 Maadili 03: Mgeni rasmi Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi,  Prof. Joyce Ndalichako akisisitiza jambo kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wakati wa ufunguzi wa mdahalo wa wanafunzi kuhusu kujenga na kukuza maadili, haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU)akitoa neno la ukaribisho kwa Mgeni rasmi Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi,  Prof. Joyce Ndalichako wakati wa ufunguzi wa mdahalo wa wanafunzi kuhusu kujenga na kukuza maadili, haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi na wageni waalikwa wakimfuatilia kwa makini Mgeni rasmi Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi,  Prof. Joyce Ndalichako wakati wa ufunguzi wa mdahalo wa wanafunzi kuhusu kujenga na kukuza maadili, haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wanafunzi na wageni waalikwa wakimfuatilia kwa makini Mgeni rasmi Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi,  Prof. Joyce Ndalichako wakati wa ufunguzi wa mdahalo wa wanafunzi kuhusu kujenga na kukuza maadili, haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Sheikh Ally Mbwera toka Umoja wa Shule za Msingi za Kiislamu Tanzania akitoa mada wakati wa mdahalo wa wanafunzi  wa shule za msingi na sekondari kuhusu kujenga na kukuza maadili, haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
 Maadili 06: Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na mchambuzi wa masuala ya uongozi Binto Mawazo Binto akitoa mada wakati wa mdahalo wa wanafunzi  wa shule za msingi na sekondari kuhusu kujenga na kukuza maadili, haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi na wageni waalikwa wakimfuatilia kwa makini watoa mada wakati wa mdahalo wa wanafunzi  wa shule za msingi na sekondari kuhusu kujenga na kukuza maadili, haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi,  Prof. Joyce Ndalichako akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mdahalo wa wanafunzi  wa shule za msingi na sekondari kuhusu kujenga na kukuza maadili, haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Eliphace Marwa - Maelezo
***************************************************
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
SERIKALI imewataka wakuu wa shule za Msingi na Sekondari nchini pamoja na Bodi zake kuhakikisha wanachukua hatua stahiki dhidi ya vitendo vya utovu wa nidhamu unaofanywa na baadhi ya wanafunzi shuleni.

Agizo hilo limetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako wakati wa mdahalo kuhusu kujenga na kukuza Maadili, Haki za binadamu, Uwajibikaji, Utawala bora na Mapambano dhidi ya rushwa uliolenga kukuza na kusimamia maadili kwa vijana.

Prof. Ndalichako alisema kuwa Serikali imebaini kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya walimu kuwa bodi za shule kusita kuchukua hatua stahiki na kutetea baadhi ya wanafunzi wakorofi wanaopelekewa na kuwaacha kuendelea na masomo.

Aidha, Prof. Ndalichako aliziagiza bodi hizo kusimamia sheria, kanuni na taratibu kuhusu maelekezo mbalimbali yanayotolewa na kuachana na siasa katika suala zima la maadili kwa wanafunzi.

Prof. Ndalichako alisema suala la Maadili na makuzi kwa vijana ni suala lililopewa kipaumbele na Serikali ya Awamu ya Tano, hivyo kuwataka vijana kushirikiana ili kuweza kukuza na kusimamia suala hilo.

“Suala la kukuza na kusimamia maadili siyo jukumu la Rais pekee, au jukumu la taasisi pekee, bali ni jukumu la jamii nzima, hivyo tunatakiwa sote kushirikiana kwa pamoja katika ngazi zote”, alisema Prof. Ndalichako.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa, (TAKUKURU) Bw. Valentino Mlolowa alisema kuwa mdahalo huo unalengo la kuwawezesha wanafunzi kupata elimu kuhusu Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Utawala bora na Mapambano dhidi ya Rushwa kwa kuamini wanafunzi ni kundi lenye nguvu katika kuleta mabadiliko katika jamii.

Mlolowa alisema kuwa mdahalo huo ni sehemu ya harakati za Serikali kupitia taasisi zake za kuendeleza na kuhimiza maadili, kuchochea na kujenga uadilifu katika jamii na taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.