Habari za Punde

SIMBA NAO WAITISHA MKUTANO MKUU WA DHARURA DESEMBA 11 MWAKA HUU

Na Zainab Nyamka, Dar
KUTOKANA na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuamuru klabu za Yanga na Simba kufanya mabadiliko ya katiba, hatimaye Uongozi wa klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba wameitisha mkutano mkuu wa dharula unaotarajiwa kufanyika Desemba 11 mwaka huu.

mkutano huo wa dharula umeitishwa ikiwa ni katika mchakato wa kuingia kwenye mfumo mpya wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo ambao utahusisha moja kwa moja kubadili katiba yao.

Mkuu wa kitengo cha habari wa Simba, Haji Manara ametoa taarifa hiyo leo na kuweka wazi kuwa lengo la kufanya mkutano wa dharula ukiwa ni mlengo thabiti wa kufanya mabadiliko ya katiba ili kuweza kwenda na wakati na mchakato mpya wa uendeshaji wa klabu hiyo.

Barua hiyo rasmi iliyotolewa leo na Uongozi wa Simba baada ya kamati ya utendaji ikiongozwa na Rais Evance Aveva, imeeleza kuwa kwa pamoja Viongozi wa Klabu hiyo walikubaliana kuitisha mkutano mkuu wa dharula kwa mamlaka ya katiba yao ya Ibara ya 22 kifungu cha kwanza inayowaruhusu   na nyaraka zote za ajenda ya mkutano huo zitakabidhiwa kwa matawi kama ibara ya 22 kifungu cha nne kinavyosema.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.