Habari za Punde

SIMBA WAMGOMEA KIGANJA, WASEMA MAAMUZI YA DESEMBA 11 NI HALALI

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Haji Manara akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam
*************************************
Na Zainab Nyamka, Dar
KLABU ya wekundu wa Msimbazi Simba imesikitishwa na kauli ya Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Mohamed Kiganja kuwa mkutano wao mkuu wa dharura wa mabadiliko ya katiba kutoka katika mfumo wa uendeshaji wa wanachama na kuingia kwenye hisa uliopangwa kufanyika Disemba 11 maamuzi yake hayatakuwa na mashiko mpaka yapitishwe na Baraza hilo.

Kiganja aliyasema hayo jana wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuwa mkutano huo ni ruksa kufanyika kama utafuata sheria na taratibu zote kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo lakini mwisho wa siku maamuzi yatakayopitishwa lazima yapitie kwa msajili na baadae kufika kwa baraza hilo.

Mkuu wa Kitengo cha SIMBA WAMGOMEA KIGANJA, WASEMA MAAMUZI YA DESEMBA 11 NI HALALI na Mawasiliano wa klabu ya Simba Haji Manara amesema mkutano huo umefuata taratibu zote na maamuzi yake hayatapitia sehemu nyingine yoyote na wameshangazwa na kauli ya Kiganja kuwa hata wakijadiliana lakini maamuzi yatoke BMT na wanaiheshimu sana kwakua ipo kwa mujibu wa sheria za nchi lakini haina mamlaka ya kuingilia mambo ndani ya klabu hiyo kwakua katiba inakataza na mabadiliko ya kiundeshwaji hayaepukiki kwa namna yoyote.

"Kiganja anasema mkutano ufuate utaratibu zote kwa mujibu wa katiba yetu lakini maamuzi lazima yafike kwao wayapitie wao wakati Waziri wa Habari Nape Nnauye alisema haina shida kama mkutano upo kwa mujibu wa katiba ya Simba" amesema Manara. Alienda mbali zaidi na kusema kuwa BMT inaonekana wakati wa matatizo tu kwenye maendeleo haionekani kitu ambacho kinatia walakini.

"Mbona hawakutusaidia kuzitoa nyasi zetu bandia bandarini na vipi kuhusu mishahara ya wachezaji mbona hawatusaidii kulipa lakini kwenye Mkutano wanasema watatoa maamuzi hilo suala halipo" amesema Manara.

Ikumbukwe kuwa BMT kupitia kwa Kiganja alisitisha michakato yote ya mabadiliko ya uendeshaji wa klabu za Yanga na Simba mpaka pale watakapofanya mabadiliko ya katiba zao naanachama wote kuridhia kuimgia mfumo huo.

wakati huo huo,
Klabu ya Simba imewekwa wazi kuwa hawataimgiza timu yao uwanjani kama Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF watashindwa kuleta waamuzi kutoka nje katika mchezo wao dhidi ya Yanga raundi ya pili.

Simba wamesema kuwa msimamo wao upo pale pale na hawatabadilisha maamuzi hayo kwani waamuzi wengi wa hapa nchini wamekuwa na tabia ya kuwabeba Yanga kwenye mechi zao na raundi hii ya pili wapo tayari kulipa faini ila hawataingiza timu uwanjani.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.