Habari za Punde

SIMBA YAPUNGUZWA KASI NA WADOGO ZAO AFRICAN LYON, YAPIGWA 1-0

LILIKUWA ni bao la kiungo Abdallah Mguhi aliyetokea benchi katika dakika ya 89 liliweza kupoteza matumaini ya Mnyama Simba, kuibuka na ushindi ili kuendeleza ubabe katika mechi zake za Ligi Kuu Bara uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Bao hilo pekee katika mchezo huo limeiwezesha African Lyon kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kaka zao Simba SC na kuwasimamisha katika mbio zao za kuwakimbia Watani zao wa Jadi Yanga, ambao nao katika mchezo wao wa Leo dhidi ya Tanzania Prisons wameibuka na ushindi wa bao 1-0.

Simba hivi sasa wanabakia kileleni wakiwa na pointi 35 baada ya kucheza mechi 14 wakiwa na tofauti ya Pointi tano na wapinzani wao Yanga wenye Pointo 30 baada ya mchezo wa leo, ambao nao wakiwa wamecheza mechi 14.

Aidha Lyon leo wameweza kujiwekea Rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuwafunga Wekundu hao tangu kuanza kwa Ligi hiyo ya Bara kwa msimu huu kwa kucheza jumla ya mechi 13 bila kupoteza.

Baada ya bao hilo, Mashabiki wa Simba walianza kurusha makopo ya maji uwanjani wakionyesha kutoridhishwa na mwamuzi wa pembeni, Frank Komba wakidai kuwa mpigaji wa Krosi hiyo iliyozaa bao, Hafidh 'eti' alikuwa ameotea.

KIKOSI CHA AFRICAN LYON:
Rostand Youthe, Miraj Suleiman, Baraka Jaffar, Hamad Waziri, Isihaka Hassan, Omar Salum, Awadh Juma, Khalfan Twenye/Rehani Kibingu dk88, Hamad Manzi/Amani Peter dk63, Abdallah Mguhi ‘Messi’ na Omar Abdallah. 

KIKOSI CHA SIMBA SC:
 Vincent Angban, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shizza Kichuya, Muzamil Yassin, Mohamed ‘Mo’ Ibrahim/Ibrahim Hajib dk50, Laudit Mavugo/Said Ndemla dk81 na Mwinyi Kazimoto/Jamal Mnyate dk76.

MATOKEO MENGINE YA LIGI KUU BARA MECHI ZA LEO:
Tanzania Prisons 0 - Yanga SC 1
African Lyon 1 - Simba SC 0
Mbao Fc 2 - Azam Fc 1
Ndanda Fc 2 - Standa United 1
Kagera Sugar 3 - Ruvu Shooting 1

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.