Habari za Punde

TANESCO KIGOMA YADAIWA SHILINGI MILLIONI 49 NA TEMESA

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu ( kushoto) akizungumza na Meneja wa TEMESA Kigoma Mhandisi Hassan Karonda (kulia) alipotembelea kituoni hapo. 
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu( mwenye shati la rangi ya bluu) akijadili jambo na mafundi wa karakana ya TEMESA Kigoma alipotembelea kituoni hapo kujionea utendaji kazi. 
Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. MussaMgwatu (aliyeketi) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtaalam James Frank jinsi mfumo wa kielektroniki wa kukatishia tiketi katika kivuko cha Ilagala Mkoani Kigoma unavyofanya kazi. 
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (wa pili kulia) akiongozana na Meneja wa TEMESA Kigoma Mhandisi Hassan Karonda (kulia) baada ya kukagua kivuko cha MV. Malagarasi kinachotoa huduma ya usafiri katika Mto Malagarasi kati ya Ilagala na Kajeje mkoani Kigoma. 
Picha/habari na Theresia Mwami TEMESA kigoma
****************************************************
Shirika la umeme Tanzania TANESCO linadaiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Kigoma kiasi cha shilingi milioni 41 ikiwa ni malimbikizo ya madeni kutokana na matengenezo ya magari mbalimbali yaliyofanywa na shirika hilo mkoani humo.

Hayo yameelezwa na Meneja wa TEMESA Mkoa wa Kigoma Mhandisi Hassan Karonda alipokuwa akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu alipotembelea kituoni hapo.

Meneja huyo ameeleza kuwa kwa sasa TEMESA Kigoma ipo kaytika operesheni ya kukusanya madeni kutoka kwa Taasisi na makampuni wanayoyadai.

“Mtendaji Mkuu tunazidai Taasisi mablimbali kiwemo Shirika la Umeme Tanzania TANESCO shilling million 41 mpaka sasa” alisema Mhandisi Karonda.

Hata hivyo Dkt. Mgwatu alimtaka Mhandisi Karonda kuhakikisha kuwa anakusanya madeni yote anayodai mkoani humo haraka iwezekanavyo.

“ Fuatilia ofisi kwa ofisi kukusanya madeni ili kukiwezesha kituo hiki kufanya kazi zake kwa ufanisi mkubwa” alisisitiza Dkt. Mgwatu.

Akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo Dkt. Mgwatu pia alipata fursa ya kutembelea kivuko cha MV. Malagarasi na kuona utendaji kazi wake.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt Mussa Mgwatu yupo katika ziara ya kutembelea vituo vya TEMESA nchi nzima kujionea utendaji kazi wa vituo hivyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.