Habari za Punde

TANZIA: JOSEPH MUNGAI AFARIKI DUNIA JIONI HII


Habari zilizotufikia hivi punde kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, zinasema kuwa Aliyewahi kuwa Waziri wa elimu na Utamaduni katika Serikali ya Benjamin W. Mkapa ndugu Joseph Mungai, amefariki dunia majira ya saa 11 jioni.

Akithibitisha taarifa hizo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha, alisema kuwa marehemu Mungai alifikishwa Hospitalini hapo leo baada ya kula kitu kibaya kinachodhaniwa 'Sumu' na kutapika mfululizo hali iliyompelekea kupoteza maisha. 

Mwili wa marehemu umehifadhiwa Chumba cha maiti katika Hospitali hiyo ya Taifa ya Muhimbili.

Habari kamili ya msiba huo zitawajia kadri zitakavyokuwa zikitufikia.
Mtandao huu unatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki.Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe.
Mungu ilaze roho ya Marehemu mahala pema peponi, Amina

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.