Habari za Punde

TFF YAMPIGA PINI MCHEZAJI WA KAGERA SUGAR

Kutokana na malalamiko ya timu ya mpira wa miguu ya Panone Fc juu ya ushiriki wa mchezaji Christopher Mahanga katika Ligi ya TFF ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 iliyoko Kundi A, Kituo cha Bukoba Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limesimamisha ushiriki mchezaji Christopher Mshanga katika mashindano yanayoendelea mpaka uchunguzi wa suala lake utakapokamilika.

Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za wachezaji italifanyia kazi suala hilo na taarifa itatolewa.

Hatua ya TFF imekuja baada ya kuibuka malalamiko kutoka timu ya mpira wa miguu yaPanone ya Moshi Kilimanjaro kushangazwa na mchezaji huyo kuibukia timu ya Kagera ilihali akidaiwa kuwa na usajili katika timu hiyo kwa msimu wa pili mfululizo.

Kwa haraka, Idara ya Mashindano ya TFF imebaini kuwa mchezaji huyo alikuwa na usajili kwa timu zote mbili kwa usajili wa majina tofauti ilihali picha ikionekana kuwa mmoja.

Panone FC alisajiliwa kwa jina la Christopher Mshanga kuanzia msimu wa 2015/2016 na pia msimu wa 2016/17.

Taarifa za awali ambazo TFF ingali ikizifanyia kazi zinasema kwamba baada ya kusajili Panone FC ya Moshi, akachezea timu mbili na kuaga kuwa amekwenda kutibiwa majeraha, lakini wakati anasubiriwa, amekuja kuonena kwenye mchezo ambao Kagera ilikuwa ikicheza na Young Africans kwenye ligi ya vijana wa U20 ya TFF.

Kwa mbinu za kuchezea mtandao, mchezaji huyo pia akasajiliwa na Kagera Sugar msimu wa 2016/17 na Kagera kwa jina la Christopher Paschal Peter Mshanga.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.