Habari za Punde

WANANCHI WATAKIWA KUJIKITA KATIKA MAENDELEO BADALA YA KUENDEKEZA SIASA.

 Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu akizungumza mara baada ya kutembelea eneo la kukagulia mizgo katika Bandari ya Dar es Salaam iliyopo chini ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) alipokuwa akihitimisha ziara yake ya siku mbili leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Mhandisi Deusdedit Conatus Vitalis Kakoko.
 LN2: Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Deusdedit Conatus Vitalis Kakoko akizungumza wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu (kulia) alipotemdelea Bandari hiyo leo Jijini Dar es Salaam. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

Mkurugenzi  wa Kitengo cha Uhandisi cha Kampuni ya Tanzania International Container Terminal Services Ltd (TICS) Cornelius Kwadijk akimwelekeza Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu, namna kampuni yao inavyofanya kazi ya kutoa makontena wakati wa ziara ya Rais huyo katika Bandari ya Dar es Salaam leo.
Pichani  mtambo wa kutolea Kontena Bandarini unaomilikiwa na Kampuni ya Tanzania International Services Ltd (TICS).
Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu akionyesha zawadi aliyopewa na uongozi wa Bandari kavu ya Zambia Cargo and Logistics alipotembelea Ofisi zao za Jijini Dar es Salaam leo.Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zambia Cargo and Logistics David Chimfwembe.
 Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu(katika) akimsikiliza kwa makini Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zambia Cargo and Logistics David Chabwa Chimfwembe.Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Serikali ya Tanzania Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu(katika) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) alipotembelea katika Bandari ya Dar es Salaam leo. Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.
**********************************************
Na Beatrice Lyimo - MAELEZO 
RAIS wa Zambia Edgar Lungu amewataka wananchi kuaachana na masuala ya siasa na kujikita katika kukuza maendeleo ya uchumi wa nchi.
Rais Lungu ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati alipotembelea Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), TICTS na kampuni ya  bandari kavu ICDs  ZAMCARGO AND LOGISTIC LTD  ikiwa ni ziara yake ya siku tatu nchini Tanzania.
“Muda wa siasa umekwisha, wanasiasa wanakuja na kuondoka lakini maendeleo ya nchi yatabaki, hivyo kikubwa tujikite katika kujenga na kukuza uchumi kwa ajili ya nchi” alifafanua Rais Lungu.
Aidha, Rais Lungu amewataka wafanyakazi wa ZAMCARGO AND LOGISTICS kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kutengeneza faida kwa kampuni  kwani lengo la kuleta ushindani baina yao na makampuni mengine.
Mbali na hayo Rais Lungu aliahidi wafanyakazi hao  kuwa Serikali ya Tanzania na Zambia zitashirikiana katika kutatua baadhi ya changamoto zinazo wakabili ili kuweza kuimarisha kampuni hiyo.
Nae Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani alisema kuwa ushirikiano baina ya Tanzania na Zambia ulianza kabla ya Uhuru ambapo reli ya TAZARA ilitumika katika kuunganisha nchi hizi mbili ambazo mpaka sasa zinashirikiana katika masuala tofauti.
“Matunda ya waasisi wetu Rais Mstaafu Dkt. Kenneth Kaunda na Hayati Mwalimu Julius Nyerere yanaonekana hadi leo ambapo nchi ya Zambia na Tanzania zimeendelea kushirikiana katika masuala ya biashara na kiuchumi kwa ujumla.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Balozi  Dkt. Augustine Mahiga alisema  kuwa wananchi wa Tanzania na Zambia wataendelea kunufaika na urafiki uliopo baina yao katika masuala mbalimbali ikiwemo kiuchumi.

Katika hatua hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko alisema kuwa scana iliyokaguliwa na Rais Lungu inauwezo wa kuscani makontena 45 au magari 45 kwa saa ambapo itasaidia katika kukusanya mapato ya taifa na pia katika kuimarisha ulinzi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.