Habari za Punde

WAOGELEAJI WA DAR SWIM CLUB WAFANYA VYEMA MASHINDANO YA KENYA

Kocha wa timu ya kuogelea ya Dar Swim Club (DSC), Salum Mapunda (kushoto) akiwa na waogleaji wake kabla ya kushindana katika mashindano ya Taifa ya Kenya yajulikanayo kwa jina la Kenya National’s Age groups open and relay swimming championship. DSC ilishinda jumla ya medali tisa katika mashidano hayo.
Kocha wa timu ya kuogelea ya Dar Swim Club (DSC), Salum Mapunda akiwaelekeza waogeaji wake wakati wa mashindano ya Taifa ya Kenya yajulikanayo kwa jina la Kenya National’s Age groups open and relay swimming championship. DSC ilishinda jumla ya medali tisa katika mashidano
Waogeaji na viongozi wa Dar Swim Club wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa na kikombe, medali walizoshinda katika mashindano ya Taifa ya Kenya yajulikanayo kwa jina la Kenya National’s Age groups open and relay swimming championship. DSC ilishinda jumla ya medali tisa katika mashidano hayo.
***********************************************
Klabu ya mchezo wa kuogelea ya Dar Swim Club (DSC) imefanya vizuri katika mashindano ya wazi nay a umri ya Kenya baada ya kutwaa medali tisa, kikombe na vyeti. 

Mashindano hayo ya wazi yalifanyika mjini Mombasa na kushirikisha timu kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo, Uganda, Kenya, Swaziland na Tanzania Bara. Mbali ya DSC, klabu ya Shule ya Kimataifa ya Moshi (ISM) nayo ilishiriki katika mashindano hayo yaliyofanyika kwenye bwawa la kuogelea la Aga Khan Academy. 

Katibu Mkuu wa DSC, Inviolata Itatiro alisema kuwa mwogeleaji wake, Marin de Villard aliweze kutwaa medali saba na vyeti tisa kwa kufanya vizuri katika staili mbalimbali. Marin alishinda medali ya dhahabu katika staili ya freestyle ya mita 50 na 100 na baadaye kushinda medali ya fedha katika staili ya backstroke kwa mita 50 na 100 kwa waogeleaji wa kati ya miaka 10 na 11. 

Inviolata alisema kuwa Marin pia alishinda medali ya shaba kwa mita 100 na 200 katika staili ya Medley (IM) na vile vile kushinda mdali ya shaba katika staili ya butterfly kwa mita 100. Muogeleaji mwingine, Celina Itatiro aliweza kushinda medali mbili na vyeti nane kwa kufanya vizuri. Celina alishinda medali za sahaba katika staili za freestyle na butterfly katika mashindano ya mita 100. 

Naye Chichi Zengeni alifanya vyema na kutambuliwa kwa kupewa vyeti vinne huku akihimarisha muda wake wa kuogelea mara 10, huku Kayla Temba akihimarisha muda wake mara nane), Reuben Monyo akihimarisha muda wake mara tano na Peter Itatiro akihimarisha muda wake mara tano. 

“Tumejivunia sana matokeo haya, ni mazuri kwani waogeleaji wetu wengi wameshiriki mara ya kwanza mashidano ya kimataifa, tunachoangalia sisi ni jinsi gani muogeleaji wetu anahimarisha muda wake, kupata uzoefu na kushinda,” alisema Inviolata. 

Inviolata alisema kuwa klabu yao imedhamiria kushiriki katika mashindano mengi zaidi ya nchini na Kimataifa ili kujenga uwezo wa waogeleaji wake wachanga kwa ajili ya mashindano makubwa ya kimataifa kama Mataifa ya Afrika (All Africa Games), Jumuiya ya Madola, Olimpiki na Mashindano ya Dunia.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.