Habari za Punde

WATANZANIA WAHASWA KUEPUKA MATUMIZI YA POMBE NA SIGARA

 Mkurugenzi wa Tiba wa Wizara ya Afya, Maenedeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Magreth Mhando aliyesimama akiongea na wasimamizi wa afya  ngazi ya Mkoa na Wilaya hawapo pichani katika ufunguzi wa mkutano Utekelezaji Wa Mpango mkakati wa Huduma za magonjwa yasiyoambukiza uliofanyika mkoani Morogoro kulia ni Kaimu Mkurugenzi msaidizi wa magonjwa yasioambukizwa Shadrack Buswelu.
 Baadhi ya wadau wa afya na wasimamizi wa afya kutoka ngazi ya mkoa na wilaya wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Tiba wa Wizara ya Afya, Maenedeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Dkt. Magreth Mhando hayupo pichani.
Kaimu Mkurugenzi msaidizi wa magonjwa yasioambukizwa Shadrack Buswelu kushoto akiongea na waandishi wa habari katika ufunguzi wa mkutano wa Wa Utekelezaji Wa Mpango mkakati na Huduma za magonjwa yasiyoambukiza uliofanyika mkoani Morogoro.
******************************************************************
Na Ally Daud-MAELEZO MOROGORO.
WATANZANIA hasa watumiaji Wa pombe na Uvutaji Sigara wamehaswa kuepuka matumizi hayo kwani yanachangia kuongeza magonjwa  yasiyoambukiza ili kusaidia kupunguza asilimia 1.5 ya vifo vinavyotokana na magonjwa hayo kwa kukinga, kutibu na kuzingatia afya ya akili  kufikia mwaka 2030.
Akizungumza hayo kwenye ufunguzi Wa mkutano Wa Utekelezaji Wa mpango mkakakti na Huduma za magonjwa yasiyoambukiza kwa madaktari na watoa huduma za afya  ngazi ya mkoa na wilaya Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Magreth Mhando Mkoani Morogoro.
"Watanzania wanatakiwa kuepuka matumizi ya unywaji pombe na uvutaji wa Sigara kwa wingi ili kuepuka magonjwa yasioambukizwa na kutokomeza vifo vinavyosababishwa na magonjwa hayo ili kujenga taifa lenye afya imara na uchumi mzuri" alisema Dkt. Mhando

Aidha Dkt. Mhando amesema kuwa idadi ya watu wanaotumia pombe imefikia asilimi 29.3 na wanaovuta sigara imefikia asilimia 15.9 , wenye uzito kupita kiasi asilimia 34.7 ikiwa imeongeza idadi ya wagonjwa wa shinikizo la damu kwa asilimia 25.9 na kisukari asilimia 9.1 kutoka asilimia moja mwaka 2012.

Mbali na hayo Dkt. Mhando amesema kuwa malengo ya mkutano huo ni kuhakikisha wanapata ufumbuzi wa kina na kuadhimia kupunguza nusu ya vifo vinavyotokana na ajari za barabarani nchini kufikia 2020 ili kutimiza  mpango wa maendeleo wa SDG mwaka 2030 .

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi msaidizi wa magonjwa yasioambukizwa Shadrack Buswelu amesema kuwa watanzania wanatakiwa kuepuka ulaji usiokua na tija na wajikite kwenye mazoezi ya mara kwa mara  ili kuepuka magonjwa yasioambukiza na kujenga taifa lenye watu shupavu kwa maendeleo ya nchi.
“Watanzania tunatakiwa kuepuka ulaji usio na tija na tufanye mazoezi ya mara kwa mara ili kuepuka magonjwa yasioambukiza na kujenga taifa lenye watu imara kwa maendeleo yetu” alisema Bw. Buswelu.

Mkutano huo wa siku tatu unahudhuriwa na watoa huduma za afya ngazi ya mkoa na wilaya pamoja na taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali unalenga kuweka mkakati wa kupambana na magonjwa yasioambukiza kama vile kisukari , shinikizo la damu, uzito kuzidi kiasi na ajari za barabarani mpaka kufikia 2020.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.