Habari za Punde

WAZIRI UMMY MGENI RASMI KONGAMANO LA AFYA TANZANIA.

Na Ally Daud, MAELEZO, Dar es Salaam
WAZIRI  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la tatu la kitaifa la Afya litakalofanyika Novemba 14 mwaka huu Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Rais wa Kamati ya maandalizi  ya mkutano huo, Dkt. Omary Chillo  wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam wenye lengo la kujadili maendeleo ya sekta afya nchini.

Aidha Dkt. Chillo alisema kuwa  kongamano hilo litajadili jitihada ilizofikia  Tanzania katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya kimkakati ya maisha yenye afya njema (SDG-3) yaliyokusudiwa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya  wachapakazi.

Dkt. Chillo aliongeza kuwa kongamano hilo pia linatarajia kujadili mikakati ya kuboresha sheria ya usalama na afya makazini, kanuni na ufanyaji kazi nchini kwa  ajili ya maendeleo ya wafanyakazi na usalama wao.

Kwa mujibu wa Dkt. Chillo alisema kuwa kongamano hilo pia linatarajiwa kufanyika kuwakutanisha wataalam wa sekta ya afya 700 na kuratibiwa na taasisi tano zikiwemo MoHCDGEC, TMHS,APHFTA,CSSC na BAKWATA.

Mkutano  huo ambao utakutanisha taasisi 53 za afya, zinatarajia pia  kushiriki katika maonesho  ya bidhaa zinafanyika kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto pamoja na TAMISEMI tangu kuanza kwake 2014.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.