Habari za Punde

WAZIRI WA UTAMADUNI NA SANAA WA AFRIKA YA KUSINI ATEMBELEA MAZIMBU CAMPUS MKOANI MOROGORO NA KUTEMBELEA MAKABURI YA WAPIGANIA UHURU WA AFRIKA YA KUSINI

  Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa akisalimiana na Mkurugenzi wa SUA Solomon Mazimbu Campus Prof.Yasinta Muzanila alipowasili kutembelea eneo lililopo Mkoani Morogoro ambalo wapigania uhuru wa Afrika ya Kusini walilitumia katika harakati za kupigania uhuru wao na ukombozi wa bara la Afrika kwa ujumla.
 Mkurugenzi wa SUA Solomon Mazimbu Campus Prof.Yasinta Muzanila(kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa(kushoto) kuhusu Mazimbu campus na kumbukumbu zilizopo  wakati Waziri huyo alipotembelea eneo hilo liliopo Mkoani Morogoro ambalo wapigania uhuru wa Afrika ya Kusini walilitumia katika harakati za kupigania uhuru wao na ukombozi wa bara la Afrika kwa ujumla.
Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa (aliyenyoosha mkono) akiangalia moja ya makaburi ya waliopigania uhuru wa nchi yake yaliyopo Mazimbu Campus Mkoani Morogoro.
 Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa akiwa katika eneo lililowekwa sanamu ya Rais wa kwanza Afrika ya Kusini Hayati Nelson Mandela kama ukumbusho wa wapigania uhuru wa Afrika ya Kusini Mazimbu Mkoani Morogoro.
Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa akiangalia mti uliopandwa na moja wa viongozi wa Afrika Kusini kama kumbukumbu kwa  wapigania uhuru wa Afrika ya Kusini Mazimbu Campus Mkoani Morogoro.
  Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa akiweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya makaburi ya waliopigania uhuru wa Afrika ya Kusini yaliyopo Mazimbu Mkoani Morogoro.
 Moja ya alama zilizowekwa na mmoja wa viongozi wa Chama cha ANC Bw. Oliver Tambo ikiwa ni kumbukumbu ya mashujaa ya waliopigania uhuru wa Afrika ya Kusini.
Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Mazimbu Campus na ujumbe kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakati alipotembelea eneo hilo katika ziara yake hapa nchini. Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.