Habari za Punde

YANGA YAPUNGUZWA KASI YA UBINGWA NA MBEYA CITY, YAPIGWA 2-1, SIMBA YAZIDI KUJICHIMBIA KILELENI

Mabao mawili ya kipindi cha kwanza yameiwezesha Mbeya City kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kuwasimamisha Yanga katika mbio za kumfukuza mpinzani wake na mtani wake wa jadi, Simba ambaye leo ameendelea kujishindilia kileleni kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stand United katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga leo jioni. 

Bao la kufutia machozi la Yanga lilifungwa na Donald Ngoma akimalizia pasi nzuri ya Simon Msuva, huku mabao yote ya timu hizo yakifungwa katika kipindi cha kwanza.

Bao pekee katika mchezo wa Stand United dhidi ya Simba,lilifungwa na Shizya Kichuya kwa mkwaju wa penati katika kipindi cha kwanza.

MATOKEO MENGINE YA MECHI ZA LIGI KUU BARA LEO
Mbeya City 2 - Yanga SC 1
Stand United 0 - Simba SC 1
Toto African 0 - Azam Fc 1
Majimaji 1 - JKT Ruvu 0
Ndanda Fc 1 - Tanzania Prisons 0
Ruvu Shooting 1 - African Lyon 0

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.