Habari za Punde

YANGA YAWAKALISHA RUVU SHOOTING UWANJA WA UHURU 2-1

TIMU ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, leo jioni imemaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara kwa kuwachapa Ruvu Shooting mabao 2-1 na kufikisha jumla ya pointi 33 wakiwa nafasi ya pili nyuma ya Vinara wa Ligi hiyo Simba wenye Pointi 35.

Katika mchezo huo Ruvu walikuwa kwanza kupata bao dakika ya saba kupitia kwa Abrahman Mussa ambalo lilidumu hadi dakika ya 31 Yanga walipopata bao la kuswazisha kupitia kwa Simon Msuva, aliyeitendea haki pasi nzuri ya Haruna Niyonzima.

Huku Ruvu wakionekana kujenga Ukuta mgumu kwa wachezaji wote kurudi nyuma na kushambulia kwa kushitukiza, Yanga walionekana kushambulia zaidi na kufika langoni kwa wapinzani kila dakika.

Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko zilikuwa sare ya 1-1, hadi kipindi cha pili, Nahodha wa Yanga alipowainua tena mashabiki vitini kwa kuandika bao la pili na la ushindi kwa timu yake, lililodumu hadi kumalizika kwa mchezo huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.