Habari za Punde

30 WAHOFIWA KUFA MAJI ZIWA ALBERT, NCHINI UGANDA

WATU 30 wanahofiwa kufa maji baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama katika Ziwa Albert nchini Uganda jana.

Boti hiyo iliyodaiwa kuwa ilikuwa imebeba wachezaji na mashabiki waliokuwa wanakwenda kwenye mchezo wa mpira wa miguu maaluum kwa ajili ya sikukuu ya Krismasi katika Wilaya ya Hoima wakitokea mji wa Buliisa nchini humo.

Taarifa za Polisi zimeeleza kuwa boti hiyo ilikuwa na watu wapatao 45 inadaiwa kuwa ilizama baada ya abiria wote kuegemea upande mmoja wa boti. Idadi hiyo kubwa ya abiri imezidi uwezo wa boti hiyo kubeba.

Taarifa zinasema kuwa miili ya watu 9 imepatikana huku wengine 15 wakiokolewa huku wengine 21 wakiwa hawajulikani walipo.

Ajali za kuzama kwa boti katika ziwa Albert zimekuwa zikitokea mara kwa mara ambapo chanzo kikubwa kinadaiwa ni ubovu wa boti pamoja na kuzidisha abiria.

Mwezi wa 11 watu wengine 11 walifariki baada ya kuzama katika Ziwa Albert.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.