Habari za Punde

ALI KIBA, LADY JAY DEE WANG'ARA TUZO ZA EATV 2016

Waziri wa Habari, Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiwapongeza Wasanii mbalimbali waliojinyakulia tuzo zao usiku wa leo,zilizofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar,ambapo Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba ameibuka kinara kwa kujinyakulia tuzo tatu.
Mwanamuziki Ali Kiba akipokea tuzo yake ya ushindiwa Wimbo Bora wa Mwaka kutoka kwa Nandi Mwiyombela kutoka kampuni ya Vodaco Tanzania katika Tuzo za Muziki za EATV AWARDS zinazofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akikabidhi Tuzo ya Heshima kwa DJ Boniventura Kilosa aka Bony Love baada ya kutangazwa mshindi wa heshima katika tuzo za EATV AWARDS 2016 zilizofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Malimani City jijini Dar es salaam.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Lady Jay Dee akipongezwa na Mpenzi wake mara baada ya kupokea tuzo yake katika hafla ya utoaji wa tuzo za EATV AWARDS zilizofanyika kwenye ukumbi wa Malimani City jijini Dar es salaam jana usiku.
DJ Boniventura Kilosa aka Bony Love akipongezwa na DJ John Dilinga mara baada ya kupokea tuzo yake ya Heshima katika tuzo zilizoandaliwa na Kituo cha Televisheni cha EATV.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Lady Jay Dee akitumbuiza katika tuzo hizo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa EATV, Bi. Regina Mengi ambao ndyo waandaaji wa tuzo hizo.
Waziri wa Habari, Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na Wasanii mbalimbali waliojinyakulia tuzo zao usiku wa leo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.