Habari za Punde

BALOZI KIJAZI: SERIKALI ITAPAMBANA NA RUSHWA ZA KILA HAINA ILI KUJENGA JAMII YENYE MAADILI.

 Katibu Mkuu Kiongozi Mwandishi Balozi John Kijazi (mwenye koti la bluu) akiongoza matembezi ya hiari ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Maadili nchini yatakayofikia kilele chake tarehe 10 Desemba 2016 katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Matembezi hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam kuanzia Viwanja vya Karimjee na kuishia Mnazi Mmoja.
 Katibu Mkuu Kiongozi Mwandishi Balozi John Kijazi (mwenye koti la bluu) akiongoza matembezi ya hiari ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Maadili nchini yatakayofikia kilele chake tarehe 10 Desemba 2016 katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Matembezi hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam kuanzia Viwanja vya Karimjee na kuishia Mnazi Mmoja. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

 Katibu Mkuu Kiongozi Mwandishi Balozi John Kijazi (mwenye koti la bluu) akishiriki katika mazoezi ya viungo baada ya kumaliza matembezi ya hiari ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Maadili nchini yatakayofikia kilele chake tarehe 10 Desemba 2016 katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Kiongozi Mwandishi Balozi John Kijazi akihutubia washiriki wa matembezi ya hiari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza matembezi hayo leo Jijini Dar es Salaam. Matenbezi hayo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Maadili nchini yatakayofikia kilele chake tarehe 10 Desemba 2016 katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa Mussa Assad akizungumza mbele ya mgeni rasmi Balozi John Kijazi (hayupo pichani) mara baada ya kumaliza matembezi ya hiari  leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu Ikulu Peter Ilomo. Matenbezi hayo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Maadili nchini yatakayofikia kilele chake tarehe 10 Desemba 2016 katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu, Bw. Valentino Mlowola akifafanua jambo wakati mara baada ya kumalizika kwa  matembezi ya hiari leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Mwandishi Balozi John Kijazi na  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa Mussa Assad. Matenbezi hayo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Maadili nchini yatakayofikia kilele chake tarehe 10 Desemba 2016 katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Kamishna wa Maadili Bw. Waziri Kipacha akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Balozi John Kijazi mara baadaa ya kuhitimisha matembezi ya hiari leo Jijini Dar es Salaam. Matenbezi hayo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Maadili nchini yatakayofikia kilele chake tarehe 10 Desemba 2016 katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Kiongozi Mwandishi Balozi John Kijazi (mwenye koti la bluu) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na watumishi kutoka Taasisi zinazosimamia maadili, uwajibikaji, Utawala Bora, haki za binadamu na mapambano dhidi ya rushwa.mara baada ya kumaliza matembezi ya hiari ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Maadili nchini yatakayofikia kilele chake tarehe 10 Desemba 2016 katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Mwandishi Balozi John Kijazi (mwenye koti la bluu) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi kutoka Taasisi zinazosimamia maadili, uwajibikaji, Utawala Bora, haki za binadamu na mapambano dhidi ya rushwa pamoja na watoto mara baada ya kumaliza matembezi ya hiari ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Maadili nchini yatakayofikia kilele chake tarehe 10 Desemba 2016 katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Picha zote na: Ally Mataula – Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
************************************************************************
Na Joseph Ishengoma
Serikali imesema kuwa imedhamiria kwa dhati kupambana na rushwa za kila aina ili kujenga jamii yenye maadili na inayochukia vitendo vya rushwa.
Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Mwandisi Balozi John Kijazi amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akihitimisha matembezi ya watumishi wa taasisi zinazosimamia maadili, uwajibikaji, utawala bora, haki za binadamu na mapambano dhidi ya rushwa.

Matembezi hayo yameanzia katika viwanja vya Karimjee hadi Mnazi Mmoja  na kuzishirikisha taaasisi zinazohusika na masuala ya utawala bora.
Taasisi hizo ni Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa, mamlaka ya kudhibiti manunuzi ya umma, na ofisi ya Taifa ya ukaguzi wa hesabu.

Taasisi nyingine ni Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Tume ya Utumishi wa Umma, na Tume ya Haki za Binadamu.
“Ipo mifano ya sehemu ambazo rushwa imekithiri kutokana na vitendoi vya rushwa na ufisadi. Kiongozi mkubwa anashindwa kumsimamia mtu aliyechini yake kama sheria ya maadili inavyomtaka kwasababu yeye mwenyewe mikono yake si misafi,” amesema na kuongeza kuwa , “matokeo yake hata mtu awe na mali nyingi, bado ataendelea kula rushwa bila kikomo”.

Balozi Kijazi amesema, “serikli ya awamu ya tano imedhamiria kupambana na rushwa ya aina zote kwa lengo la kujenga jamii yenye maadili inayochukia vitendo vya rushwa na ufisadi.”
Kwa mujibu wa Balozi Kijazi,  jitihada za serikali ni kuondokana na hulka ya ubinafsi na uroho na kujenga utamaduni na tabia ya kijitolea.”

Aidha Katibu Mkuu Kiongozi ametoa wito kwa waandishi wa habari na vyombo vya habari kuonyesha uzalendo kwa kuielimisha jamii kuhusu maswala ya maadili nchini.
“Natoa wito kwa waandishi wa habari na vyombo vya habari kuonyesha uzalendo kwa taifa letu kwa kuielimisha jamii kuhusu kujenga, na kukuza maadili, haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bola na mapambano dhidi ya rushwa,” amesema.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna Valentino Mlowola ameeleza kuwa lengo la matembezi hayo ni kutuma ujumbe kwa wananchi kuhusu kujenga na kukuza maadili, haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa.

Kamishna Mlowola amesema, kuanzia Jumatatu ijayo, taasisi zinazohusika na masuala ya utawala bora zitakuwa na wiki ya utoaji huduma katika viwanja vya Mnazi Mmoja ili kupokea kero na malalamiko ya wananchi na kisha kuyashughulikia.
“Hii ni moja ya kampeini ya taasisi husika kuikataa rushwa, kujenga maadili na misingi ya uadilifu na kuhamasisha jamii kujua haki zao,” amesema.
Kampeini hii ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu iliyoanza Novemba 10 mwaka huu ambayo kilele chake ni Desemba 10, 2016.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.