Habari za Punde

BALOZI WA UJERUMANI AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA FEDHA NA KUAHIDI KUJENGWA KWA KIWANDA KIKUBWA CHA MBOLEA MKOANI LINDI

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia) akiangalia nyaraka alizokabidhiwa na  Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bw. Egon Kochankewakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.  Kulia kwa Waziri ni Mchumi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Melckzedek Mbise na anayefuata ni katibu wa Waziri Bw. Makamba.
 Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bw. Egon Kochanke (katikati) pamoja na ujumbe wake wakisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani),  Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.
 Ujumbe wa Ujerumani ukiongozwa na Balozi wan chi hiyo nchini Tanzania, Egon Kochanke (katikati) ukiwa katika mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Kulia) wakati wa mazungumzo kuhusu uhusiano uliopo kati ya nchi hizo mbili, Jijini Dar es salaam. Kulia kwa Balozi  ni Mkurugenzi wa Ushirikiano Bi. Julia Hannig na na kushoto kwake ameketi Naibu Balozi wa Ujerumani hapa nchini Bw. John Reyels. 
 Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bw. Egon Konchanke akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) (wa pili kushoto) akielezea namna ya ushirikiano wa maendeleo kati ya nchi ya Tanzania na Ujerumani unavyoweza kuwa na tija kwa pande zote, wakati wa kikao kati yake na  Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bw. Egon Konchanke, Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi wa ushirikiano kutoka ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bi. Julia Hannig, akifafanua jambo wakati wa kikao kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Egon Kochanke (kulia), Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akiagana na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bw. Egon Kochanke (kulia) baada ya kumalizika kwa kikao kati yao, kilichofanyika  Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia) akiagana na Mkurugenzi wa Ushirikiano kutoka Ujerumani, Bi. Julia Hannig, nje ya Makao makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango baada ya kumalizika kwa mkutano katika ya ujumbe huo kutoka Ujerumani ukiongozwa na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Egon Kochanke, Jijini Dar es salaam. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Hazina

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.