Habari za Punde

BODI YA WADHAMINI SIMBA KUTOA TAMKO KESHO

Na Zainab Nyamka, Dar
KUELEKEA Mkutano mkuu wa dharula uliotishwa na Kamati ya Utendaji ya Simba ikiongozwa na Rais Evance Aveva, bodi ya wadhamini wa timu hiyo imeamua kujitokeza hadharani na kuongelea mikakati ya timu yao kuelekea duru la pili la Ligi Kuu Vodacom Desemba 17.

Bodi hiyo, ikiongozwa na Mwenyekiti Mzee Hamisi Kilomoni, itazungumza na waandishi wa habari na kuelezea mikakati yao ya kuhakikisha timu hiyo inaendelea kufanya vizuri pamoja na kuwaeleza wanachama wa timu hiyo masuala mazima ya timu yao.

Mkutano huo unaotarajiwa kuwa kesho, unaweza kuwa pia ni msumari kwa uongozi wa Simba kuelekea mkutano mkuu kwani Mzee Kilomoni amesema kuwa wao kama bodi ya wadhamini hawana taarifa yoyote ya mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.