Habari za Punde

BONDIA FRANCIS CHEKA AGOMA KUPANDA ULINGONI KESHO KUMKABILI DULLAH MBABE


Habarini za jioni mashabiki wangu poleni sana na majukumu Nipo Dar es Salaam Napenda kuwajulisha kuwa kesho SITAPANDA ULINGONI kupambana na Dullah Mbabe, ifahamike hivyo na maamuzi haya nimeamua kwa kushirikiana na Management yangu baada ya muandaaji wa pambano hilo 'Promota' kutoonyesha ushirikiano.

Ngumi ndio kazi yangu napigana ili nipate pesa sasa mtu anaandaa pambano halafu pesa ya kumlipa bondia ili apande ulingoni haijamaliziwa kwangu mpaka sasa na leo siku ya kupima uzito ndio ilitakiwa nimaliziwe malipo yangu lakini hakuna kilichofanyika, utaratibu wangu wa kazi huwa sipandi ulingoni bila kulipwa pesa yangu na huwa siupi nafasi ubabaishaji katika kazi yangu.

Kwa hiyo mashabiki wangu kama mtapenda mnaweza kujitokeza PTA kuwaona mabondia wengine watakaopanda ulingoni.

Nawaombeni radhi mashabiki wangu nipo tayari kupigana kwa siku nyingine yoyote atakapomalizia malipo yangu.

Nawatakieni sikukuu njemaa ya xmass na mwaka mpya.

Ahsanteni sana.

mwisho wa kunukuu ujumbe wa Bondia huyo Frncis Cheka aliouandika katika ukurasa wake wa Face Book hii leo akithibitisha kutopanda ulingoni kesha kumkabili Dullah Mbabe.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.