Habari za Punde

BONDIA FRANCIS CHEKA AIBUKA NA MPYA 'ETI SAINI YAKE IMEGUSHIWA' KATIKA MKATABA WA PAMBANO ALILOLIKACHA

Ninaposema mkataba umegushiwa namaanisha hivyo hapo chini,
Angalieni saini zangu za passport na visa za hivi karibuni, na linganisha na sahihi iliyopo kwenye mkataba wa promota,  Je vinaendana?


Na mjue kuwa liliandaliwa pambano na Mthailand mwaka jana na promota huyo Siraju Kaike, mimi nilipewa mkataba wa sh Million 6, baada ya Mechi nikapewa Sh 50,000 tu, sijalipwa deni langu mpaka leo nadai,  je wewe kama mshabiki na Mdau wa ngumi ungepanda tena ulingoni bila kupewa hela yako tena?


Na mkataba niliosaini ni kucheza Morogoro, ilikuwa ni ubinadamu kwenda Dar maana Dullah ndio alichotaka, sina mkataba wa PTA, na kama kuvunjika ulianzia hapo...


TPBC mtumie weledi na sio kuwahi kusikika habarini...


Na kwa bahati mbaya, mchezo wa Juzi bondia kama Twaha Khassim(Kiduku) mpaka sasa hajalipwa hela yake kamili na huyo Promota Kaike, na ni ndogo sana, Je hiyo yangu ndio angelipa?
Wakuwajibishwa ni nani hapo, Promota au mimi nae onewa? Ally Bakari, Chaurembo Palasa


HAYA NI MANENO YAKE ALIYOANDIKA KATIKA UKURASA WAKE WA FACE BOOK

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.