Habari za Punde

BREAKING NEEEEEWZZZZZ!!!!.....DKT. MAGUFULI AFANYA UTEUZI MPYA NDANI CCM, AMTEUA POLEPOLE KUCHUKUA NAFASI YA NAPE


Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameteua wafuatao kujaza nafasi mbalimbali ndani ya sekretarieti ambazo zimekuwa wazi kutokana na waliokuwa wakizishikilia kupewa majukumu mengine ya kiserikali.


Ndg. Rodrick Mpogolo anakuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndg. Rajabu Luhwavi ambaye ameteuliwa kuwa balozi.
Col. Ngemela Eslom Lubinga- Kuwa Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dr. Asha-Rose Migiro aliyeteuliwa kuwa Balozi.
Humphrey Polepole kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Ndg. Nape Nnauye aliyeteuliwa kuwa Waziri.
Wajumbe wengine watabaki kama walivyo sasa.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli,katika kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC kabla ya kufunguliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC kabla ya kufunguliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam.

Pichani kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Philip Mangula pamoja na Makamu Mwenyekiti wa (CCM Zanzibar) Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, kabla ya kuanza kikao hicho jijini Dar es Salaam.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akiwahutubia kabla ya kufungua rasmi Kikao hicho leo jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya Wajumbe waliohudhuria kikao hicho cha NEC wakifatilia kwa makini Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC wakimkaribisha Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kufungua rasmi Kikao hicho leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.