Habari za Punde

DIRISHA DOGO LA USAJILI LIGI KUU BARA KUFUNGWA SAA SITA USIKU WA LEO

Na Zainab Nyamka, Dar
DIRISHA dogo la Usajili wa Ligi Kuu Tanzania bara linatarajiwa kufungwa usiku wa leo huku Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini 'TFF' likiweka wazi msimamo wao wa kuwakumbusha klabu za ligi kuu, ligi daraja la kwanza, ligi daraja la pili kukamilisha usajili wao mapema kabisa.

Ofisa wa habari wa TFF, Alfred Lucas amesema kuwa dirisha litafungwa saa sita kamili usiku na hawatapokea tena kwani walishaweka wazi kuwa klabu zinatakiwa kuhakikisha wanafanya usajili kwa wakati na kuuwasilisha ili kuepuka usumbufu.
Lucas amesema kuwa, dirisha litakapofungwa hakutakuwa na msalie mtume kwa klabu yoyote ile kwani walishapata maelekezo toka awali. 

Dirisha la usajili lilifunguliwa mapema Novemba 15 na litafungwa leo Desemba 15 huku klabu za Simba, Yanga na Azam kufanya mabadiliko kwenye timu zao kwa kuwaacha na kupata nyota wengine wa kigeni.

Mpaka kufikia mda huu Klabu ya Yanga imemuacha nyota wake Mbuyi Twite aliyesajiliwa Majimaji ya Mjini Songea , Azam wamemuacha Pascal Wawa aliyerudi kukipiga kwenye timu yake ya zamani, Jean Mugiraneza akipara timu nchini Vietnam pamoja na kumfungashia virago pacha wake na Kipre Tcheche, Kiungo Kipre Balou.
Kwa upande Simba, Uongozi bado haujaweka wazi nani anaachwa na nani baada ya kufanya usajili wa wachezaji wawili wa kigeni akiwemo golikipa Daniel Agey na Kiungo James Kotei.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.