Habari za Punde

ITC YA NGASA YATUA MBEYA CITY


Baada ya kususua kwa takribani majuma mawili sasa hatimaye hati ya uhamisho ya kiungo Mrisho Khalfan Ngassa imetua kwenye klabu ya Mbeya City fc asubuhi ya leo .

Akizungumza na mtandao huu. Mwenyekiti wa City, Mussa Mapunda amethibitisha kutua kwa ITC hiyo kutoka shirikisho la soka la Oman ikiwa ni siku chache baada ya klabu ya Fanja kumruhusu Mrisho Khalfan Ngassa kujiunga na kikosi cha City, ambayo pia inajulikana kama timu ya kizazi kipya.

Ni kweli tumeipata, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa shirikisho la soka nchini,TFF, cham cha mpira cha Oman, hakika wamefanya kazi kubwa kufanikisha kupatikana kwa ITC hii na pia naishukuru Fanja Fc na watendaji wote kwenye timu yetu, tumekuwa na mawasiliano mazuri muda wote mpaka tumefanikiwa alisema.

Akiendelea zaidi, Mapunda alisema kuchelewa kufika kwa ITC hii hakukuwa na msuguano wowote baina ya vilabu hivi viwili kilichokuwa kinatokea ni tofauti ya wakati na siku za ufanyaji kazi kwenye ofisi kulingana na taratibu za nchi hizi mbili.

Hakukuwa na msuguano wowote uliosababisha kuchelewa kwa ITC hii, kilichokuwepo ni utofauti wa taratibu za kiofisi mara nyingi Oman siku za Ijumaa na jumamosi inakuwa ni mapumiko na huku kwetu Jumapili inakuwa mapumziko, hapo ndipo palikuwa panatuletea mpishano, jambo jema ni kuwa tayari tumeipata na tunaweza kumtumia mchezaji kwenye michezo yote ya ligi na ingine ambayo inaihusu klabu yetu alisema.

Katika hatua nyingine Mapunda amesema kuwa maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya Mbao fc uliopangwa kuchezwa jumamosi kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa yanaenda vizuri huku imani kubwa kwa uongozi wa City ikiwa ni kushinda mchezo huo hasa baada ya suluhu katika michezo miwili iliyopita.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.