Habari za Punde

KATIBU MKUU WA TIMU YA RYHNO RANGERS ATUPWA 'JELA' MIEZI MITATU

KATIBU Mku wa klabu ya Rhino Rangers, Dickson Cyprian Mgalike amefungiuwa miezi mitatu kwa kosa la kuidanganya kamati kwa kutoa taarifa potofu katika barua aliyoiandikia Bodi ya Ligi.

Maamuzi hayo yametolwa na Kamati ya usimamizi na uendeshaji baada ya kupitia ripoti nzima na kugundua kuwa Mgalike aliwadanganya na imeamua kumpa adhabu ya Kumfungiwa miezi mitatu.Hapo awali, Kamati ilimuadhibu Mchezaji Sameer Mwinyishere kwa kosa la kumrushia chupa ya maji mwamuzi.

Katibu aliandika barua kusema kwamba Sameer hakufanya kosa hilo na alimtaja mchezaji Yusuf Mputa kwamba ndiye aliyefanya kitendo cha utovu wa nidhamu kwa kumrushia Mwamuzi chupa ya maji.

Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji kwa kushirikiana watendaji wa Bodi ya Ligi ilifanya uchunguzi na kubaini mchezaji Yusuph Mputa hakuwepo kwenye Orodha ya Wachezaji wa siku hiyo. Adhabu hiyo imetolewa kwa kufuata kanuni ya 41(6).

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.