Habari za Punde

KERO KITUO CHA DALADALA CHA MAKUMBUSHO, JENGO LAKIBANA KITUO,UCHAFU, BARABARA MBOVU

 Na Ripota wa Sufianimafoto Blog,Dar
Jengo la Biashara lililojengwa kwenye Kituo cha Daladala cha Makumbusho hivi sasa limekuwa kero kwa Madereva wanaoingia na kutoka kituoni hapo kutokana na jengo hilo kuwa kubwa kuzidi malengo ya Kituo hicho ambacho kimezidi kuwa kidogo jambo ambalo linasababisha usumbufu kwa madereva hao.

Wakizungumza na Mtandao huu baadhi ya maereva wanaoingia na kutoka katika Kituo hicho, wamesema kuwa Jengo hilo limejengwa kubwa kuzidi mahitaji ya kituo, jambo ambalo limefanya kituo hicho kuwa kidogo kadri siku zinavyokwenda huku baadhi ya vyumba ama Vitalu katika jengo hilo vikiwa wazi kwa kukosa wapangaji wafanyabiashara.

Aidha Madereva hao walisema kuwa kero kubwa na changamoto inayowakabiei kituoni hapo ni alama Njia za kutoka na kuingia kwanai baadhi ya maderava wamekuwa wakisababisha foleni kutokana na kuingilia njia ambayo magari yatakiwa kutokea. 

''Ila hilo siwezi kuwalaumu madereva kwani hakuna alama yeyote inayomuonyesha derava kuwa anatakiwa kutumia njia flani kuingia na njia nyinngine kutokea, na hii imekuwa zaidi kwa madereva wa magari binafsi ambao wengi huwa wanapita tu hivyo hawajui waingilie wapi na watokee wapi, 

Na ndipo hukutana na madaladala aidha yakitoka ama kuingia na kusababisha msongamano wa magari kila mmoja akitaka kupita akijihisi ni haki yake kuelekea anakoelekea''. alisema dereva mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Hamza Mohamed anayefanya safari zake Makumbusho-Bunju.

Pia madereva hao walilalamikia barabara zinazoingia na kutoka katika Kituo hicho kuwa ni mbovu zikiwa na mashimo makubwa, ambayo hujaa maji nyakati za mvua na huwa na vumbi kwa nyakati za kiangazi kama hiki,jambo ambalo linawafanya wafanyabiashara za Hoteli 'Mama lishe' katika kituo hicho kuwa wakimwaga maji machafu katika barabara hizo ili kupungua vumbi.

''Maji wanayomwaga humu barabarani huwa ni machafu yakiwa na maukoko ya vyakula ama waliyooshea vyombo na uchafu mwingine jambo ambalo huzifanya barabara hizi kuonekana chafu muda wote zikiwa na matope hali ya kuwa hakuna hata mvua zinazonyesha''. alisema dereva mmoja

Mbali na hayo pia Kamera ya Mafoto Blog ilinasa uchafu yaani takataka zilizokusanywa nje ya kituohicho zinazolalamikiwa na watumiaji wa kituo hicho kuwa huchelewa kuondolewa kwa wakati jambo ambalo husababasha usumbufu kwa wananchi wanaotumia kituo hicho kutokana na kutoa harufu.
 Nje ya Kituo hicho kama inavyoonekana barabara ikiwa imelowa maji yanayomwagwa na mama lishe.

Magari yakiwa yamesongamana katika Kituo hicho.
 Ndani ya kituo hicho 
Baadhi ya Vyumba katika kituo hicho vikiwa wazi
 Barabara za maeneo hayo zote kumwagiliwa maji kama hivi
 Si kwamba mvua imenyesha la hasha ni wafanyabiashara za vyakula wasamalia wema eneo hili waliofanya kazi hii ya kulowesha barabara kwa maji yao machafu ili kuondoa vumbi. Lakini pia pamoja na kuondoa vumbi miundombinu ya maeneo haya ni mabovu kiasi kwamba hata barabara hizi zingekuwa na lami hawa wafanyabiashara wangemwaga wapi maji yao machafu???
 Takataka zinazolalamikiwa na wananchi na watumiaji wa kituo hicho zikiwa eneo hilo kutokana na kutoondolewa kwa wakati, huku wakilalama kuwa wao hutoa ushuru kila siku ikiwa ni pamoja na pesa za kuzolea taka hizo.
 Taka zileeeeeeeeee

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.