Habari za Punde

KONGAMANO LA BIASHARA TANZANIA NA RWANDA

Waziri wa Rwanda kizungumza wakati wa kongamano hilo.
***********************************************
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji yafungua kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Rwanda katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Maeneo Huru ya Uzalishaji (EPZA) uliopo Ubungo External. Kongamano hilo limefunguliwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. 

Injinia. Edwin Amandus Ngonyani (Aliyemwakilisha Waziri wa Viwanda) na Mhe. Waziri wa Biashara, Viwanda na Masuala ya Afrika Mashariki kutoka Rwanda Mhe. Francois Kanimba.

Aidha, Leo tarehe 08 Desemba, 2016  kutakuwa na mkutano wa pamoja (bilateral meeting) kati ya Tanzania na Rwanda kuanzia saa nne kamili asubuhi (04:00) katika ukumbi wa mikutano uliopo katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC). Mkutano huo utaongozwa na waheshimiwa Mawaziri kutoka pande zote mbili (Tanzania na Rwanda).
 baadhi ya Wajumbe walioshiriki Mkutano huo.
 Picha ya pamoja ya waheshimiwa mawaziri pamoja na wajumbe kutoka Tanzania na Rwanda.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.