Habari za Punde

MAANDALIZI YA SIKUKUU YA KRISMAS WANANCHI WAFURIKA MTAA WA KONGO DAR

 Kuelekea maandalizi ya Sikukuu ya Krismas wakazi wa Jijini Dar es Salaam, wamesongamana katika mitaa ya Kongo, Kariakoo kutafuta mahitaji ya nguo na mengineyo pamoja na kwamba kila mwananchi huimba wimbo mmoja tu kwa sasa 'Pesa hakuna'. lakini kwa msongamano huu katika kipindi hiki inaonyesha kuwa kila mwananchi alijinyima na kuzichanga kwa ajili ya Sikukuu pamoja na kwamba wale wenzetu Wachaga wao wengi wao mwaka huu hawakuweza kusafiri kutokana na hali ngumu ya upatikanaji wa pesa kama ilivyokuwa kwa miaka mingine.
 Msongamano wa raia wakisongamana kutoka barabara ya Uhuru kuingia Mtaa wa Kongo.
 Wananchi wakichagua nguo
 Mtaa wa Kongo
 Ni Bampa to Bampa

Msongamano wa wananchi wakazi wa jijini Dar es Salaam, wakiwa bize kuchagua nguo mtaa wa Kongo kuelekea Sikukuu ya Krismas.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.