Habari za Punde

MAMIA WAMUAGA MZEE MZIMBA WA YANGA, AZIKWA KIJIJINI KWAKE MSOGA

Mwili wa Marehemu Mzee Yusuph Mzimba ukisafirishwa kwenda Msoga Chalinze kwa maziko. Kwa mujibu wa mtoto wa Marehemu, Bw. Kampira, amesema kuwa Rais mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwaongoza waombolezaji katika maziko yatakayofanyika katika makaburri ya Familia uko kijiji kwake.
Kisomo katika msiba wa Mzee Yusuph Mzimba huko Magomeni Kwa Bi Nyau jijini Dar es salaam kabla ya mwili wake kuswaliwa na kisha kupelekwa kijijini kwake Msoga, Chalinze, Mkoa wa Pwani kwa Mazishi leo Desemba 4, 2016.
Mzee Ibrahim Akilimali akimzungumzia marehemu Yusuf Mzimba huko Msoga kabla ya Mazishi.
Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Bw. Imani Madega wakiwa msibani Msoga. Kushoto kwake ni Rais wa TFF Bw. Jamal Malinzi na kulia kwake ni Mzee Ibrahim Akilimali na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Majid Mwanga (kushoto)
Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili msibani kijini Msoga.
Waombolezaji wakimalizia mazishi ya Mzee Yusufu Mzimba katika makaburi ya familia yake kijini Msoga jioni hii.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.