Habari za Punde

MATUKIO KATIKA PICHA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 55 YA UHURU WA TANZANIA


Makomandoo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wakionyesha uwezo wao wa kukabiliana na adui bila kutumia silaha za moto katika maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Desemba 9, 2016. 
Makomandoo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wakionyesha uwezo wa miili yao kuvumilia maumivu kwa mmoja wao kulalia misumari huku mwenzie akimkandamiza kwa miguu katika maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Desemba 9, 2016. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi waliohudhuria sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama wakati wimbo wa Taifa ulipokuwa ukipigwa uwanjani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride katika sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Vikosi mbalimbali vya Majeshi vikipita mbele ya mgeni Rasmi kwa mwendo wa pole na Haraka katika sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli (katikati) pamoja na Viongozi mbali mbali wa Kitaifa wakisimama kupokea salama ya heshma ya Vikosi vya Ulinzi na Usalama kwa Gwaride la mwendo wa haraka katika sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam
Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ kikipita katika Jukwaa kubwa la Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo kiowanjani hapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli
Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Makomando maalum wanamaji (Marine Special Forces) kikipita katika Jukwaa kubwa la Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,kwa mwendo wa kurukaruka katika sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo kiwanjani hapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli
Vijana wa Vikosi mbali mbali vya majeshi ya Ulinzi wakiimba kwaya ya wimbo maalum katika sherehe za sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dae es Salaam, mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza na Viongozi,Wananchi na wageni mbali mbali katika sherehe za sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli alipokuwa akiagana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein baada ya kuzungumza na Viongozi, Wananchi na wageni mbali mbali katika sherehe za sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.