Habari za Punde

MBUNGE WA ARUSHA MJINI MHE GODBLESS LEMA ANYIMWA TENA DHAMANA

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imemnyima dhamana Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Mhe. Godbless Lema. Mahakama hiyo imeeleza kuwa mawakili wa mtuhumiwa huyo walipaswa kuonesha kusudio la kukata rufaa ndani ya siku 10 kabla ya kukata rufaa.

Hii ni mara ya tano mbunge huyo anakosa dhamana mahakamani tangu alipokamatwa Novemba 3 mwaka huu akiwa mjini Dodoma na kusafirishwa hadi Arusha katika kesi ya uchochezi inayomkabili.
Kesi hiyo itatajwa tena February 2, 2017.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.