Habari za Punde

'MGOMO WA YANGA UMELIPA' LYON WATUMIA FURSA WALAZIMISHA SARE 1-1


Winga wa yanga Simon Msuva akijikunja kupiga krosi ya shuti huku akizongwa na beki wa African Lyon, Hassan Isiahaka, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, jioni ya leo. 
**************************************** 
WAZEE wa 'mgomo' timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, ambao siku mbili kabla ya mchezo wao wa leo waliliripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kugomea mazoezi hadi pale viongozi wao walipotolea ufafanuzi jambo hilo,leowamelazimishwa sare ya bao 1-1 na Afirican Lyon kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es salaam. 

Baada ya matokeo hayo baadhi ya mashabiki wao walionekana kushikwa na hasira uwanjani hapo na wengine wakisikika kuwashutumu wachezaji hao kwa kugomea mazoezi na kutoka sare na Lyon huku wakibaki katika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi, wakiwa nyuma ya watani zao kwa tofauti ya Pointi 1.

Aidha baada ya mchezo wa leo Yanga wamejiongezea pointi moja na kufikisha  pointi 37 wakicheza mechi 17 sawa na Simba walio kileleni na wakiwa na pointi zake 38, ambazo zinaweza kuongezeka na akutengeneza tofauti ya nne iwapo Simba watafanikia kushinda katikamchezo wa kesho dhidi ya JKT Ruvu.


Katika mchezo huo African Lyon ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 67 kupitia kwa Ludovic Venance akimalizia pasi ya mchezaji wa zamani wa Yanga, Abdallah Mguhi ‘Messi’.Yanga walisawazisha bao hilo katika dakika ya 74 kupitia kwa Amis Tambwe , aliyeitendea haki krosi ya beki wake wa kulia Juma Abdul.Katika kile ambacho weengi hawakukitarajia na kubaki na mshangao ni mabadiliko yaliyofanya na kocha Luandamina akwa kumtoa, Thaban Kamusoko na kumuingiza Obrey Chirwa na kumtoa beki, Mwinyi Haji na kumuingiza Winga Geofrey Mwashiuya, aliyeingia na kucheza nafasi ya beki wa kushoto na kumtoa Deus Kaseke na kumuingiza
 Emmanuel Martin ambao walionyesha kubadilisha mchezo na kuongeza kasi ya mchezo.

 Amis Tambwe akiruka kupiga mpira wa kichwa kichwa katikati ya mabeki na kufunga bao la kusawazisha.
 Heka heka langoni mwa African Lyon. KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
 Kipa wa African Lyon, ... akishangilia bao lao mbele ya kamera ya Azam Tv.
 Amis Tambwe akichanja mbuga
 heka heka na apatashika uwanjani
 Kipa wa African Lyon, Youthe Jehu, akimkaba mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa,aliyekuwa akijaribu kutaka kuchukua mpira kwenye nyavu za Lyon ili kuwahisha kati baada ya kusawazisha bao, jambo ambaalo lilizua patashika langoni hapo
 Beki wa Lyon Hamad Waziri, akimkaba, Chirwa
 Deus Kasekee akijaribu kuwatoka maabeki wa Lyon
 Haruna Niyonzima akimramba chenga ya maudhi beki wa Lyon
 Heka heka langono mwa African Lyon
 Niyonzima akijaribu kumhadaa beki wa Lyon
 Beki wa Lyon akiondoka na mpira huku Msuva akilalama kuwa beki huyo aliunawa mpira
 Makocha Lwandamina na Mwambusi wakizungumza na wachezaji wao
 Mchezoaji mpya wa Yanga aliyesajiliwa dirisha dogo, akitokea KmKm ya mjini Zanzibar, 
Emmanuel Martin,akichanja mbuga
 Mwashiuya (kulia) akijaribu kumtoka beki wa Lyon
Hapa ni mpira ubaki wewe upita ama wewe ubaki mpira upite.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.