Habari za Punde

MKUU WA MKOA WA DAR, PAUL MAKONDA AMUAPISHA MKUU WA WILAYA YA UBUNGO

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akimuapisha Mkuu mpya wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Matiku Makori, wakati wa hafla hiyo ya kumuapisha iliyofanyika leo kwenye Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, zilizopo Ilala jijini.

 Mkuu mpya wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Matiku Makori, akiapa
*************************************
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amemuapisha Kisari Matiku Makori kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais Magufuli kwa Wakuu wa Wilaya hivi karibuni.

Akimuapisha Mkuu huyo wa Wilaya RC Makonda ameeleza kuwa wananchi wa Ubungo wanamatumaini na uteuzi wake na lengo kuu la kuanzisha wilaya ya Ubungo ni kusogeza huduma za wananchi karibu hivyo inabidi ahakikishe anatatua changamoto zao kwa kuwafuata huko waliko na asiridhike na ripoti anazoletewa ofisini kwani kumekuwepo na changamoto kubwa ya uwajibikaji hivyo inabidi hajiridhishe kwanza.

Katika hatua nyingine RC Makonda amewaagiza wakuu wa wilaya wote kutoruhusu wananchi kubomolewa nyumba zao mpaka kuwepo hukumu halali ya mahakama kwani wananchi wamekuwa wanaonewa na kudhulumiwa haki zao, hivyo wakuu wa wilaya kwa kushirikiana na jeshi la polisi wahakikishe haki inatendeka kwa kufuatilia ukweli na kujiridhisha kwa kuzikagua nyaraka husika.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya huyo Makori ameomba ushirikiano kwa viongozi wenzake ili aweze kutimiza majukumu yake kikamilifu na kuahidi kuwa atafanya siasa za kuleta maendeleo ili kila mwananchi anufaike na rasilimali zilizopo
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimkabidhi Katiba na Irani ya Chama cha Mapinduzi, Mkuu mpya wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Matiku Makori, wakati wa hafla ya kuapishwa zilizofanyika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ilala jijini leo.
 Baadhi ya Wakuu wa Wilaya waliohudhuria hafla hiyo ya kuapishwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kwenye Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Usalama, waliohudhuria hafla hiyo ya kuapishwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kwenye Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya akiwa katika picha ya pamoja na familia yake baada ya kuapishwa
 Picha ya pamoja na wakuu wa Usalama
 Picha ya pamoja na Wakuu wa Wilaya
 Akitia saini baada ya kuapishwa

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.