Habari za Punde

MKUU WA WILAYA KIGAMBONI KUTATUA MGOGORO WA ARDHI KATI YA WANAJESHI NA WANANCHI KESHO

  MKUU wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, anatarajia kusikiliza na kutatua kero za wananchi wake wa Kigamboni katika mkutano wa hadhara unaotarajia kufanyika kesho jumamosi eneo la Kimbiji.

Wakazi wa Kimbiji wanasumbuliwa zaidi na baadhi ya wanajeshi wenye nia ovu ya kupora ardhi na viwanja vya wananchi kwa kutumia mabavu, ambapo tatizo hilo limedumu kwa muda wa miaka tisa sasa.

Aidha wananchi hao wakazi wa Kimbiji walikwishafikisha malalamiko yao katika ngazi zote za juu bila kupata muafaka wala msaada, jambo ambalo linategemewa kutatuliwa na Mkuu huyo wa Wilaya.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.