Habari za Punde

MSANII DARASA NA WENZAKE WAPATA AJALI MKOANI SHINYANGA WANUSURIKA


 Baadhi ya Wananchi wakilitazama gari hilo baada ya kupata ajali
Muonekano wa gari alilopata nalo ajali Msanii huyo na Wenzake,
Habari zilizoifikia Globu ya Jamii hivi punde zinaeleza kuwa Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo ambaye ametokea kutikisa kwa kiasi kikubwa kupitia ngoma yake kali ya Muziki, Sharrif Thabit ‘Darassa’ amenusurika kifo baada ya kupata ajali mbaya maeneo ya Ntobo barabara ya kuelekea Mgodi wa Bullyanhulu Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Habari zimeeleza kuwa ndani ya gari hilo aina ya Toyota Harrier yenye namba za usajili T503 DGQ, ambalo dereva hakufahamika mapema, Darassa alikuwa ameambatana na Director wake, Hanscana pamoja na producer wake, Abba Process na wote wametoka salama.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Darassa amethibitisha kupata ajali hiyo, na kama aonekanavyo kwenye hiyo clip ya video sehemu ya tukio ya ajali hiyo akimshukuru Mungu kwa kutoka salama yeye pamoja na wenzake.
Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana mpaka sasa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.