Habari za Punde

MSANII MR.NICE AIBUKA NA KUFUNGUKA, AKANUSHA KIFO CHAKE

MSANII nguli wa muziki wa kizazikipya nchini, Lucas Nkenda, ameibu na kukanusha vikali habari zilizosambaa katika baadhi ya mitandao ya kijamii, zinazomzushia kifo na kusema huo ni uzushi mtakatifu.

Habazi hizo zilizosambaa zimeandikwa na Mtandao mmoja wa kijamii na katika ukurasa wa flani hivi wa Face Book, jambo liliowafanya Watanzania walio wengi kushtushwa a taarifa hizo na kubaki na maswali mengi yasiyo na majibu kuhusu taarifa hizo.

Akifunguka kwa njia ya Simu msanii huyo, Mr Nice, ambaye kwa sasa yupo nchini Kenya, amesema alishangazwa na taarifa hizo na hasa baada ya kuanza kupokea simju nyingi kutoka kwa ndugu na jamaa zake na wengi wakiuliza juu ya afya yake.

Baada ya kuona akipokea simu nyingi za usumbufu na kila moja ikiwa ni yakutaka kuthibitisha taarifa hizo, Mr Nice aliamua kuandika katika ukurasa wake wa Face Book akikanusha Taarifa hizo za uzushi.

East africa vibes nawashukuruni sana kwa kunizushia kifo sina la kuwajibu ,,ila mungu awalipe kadri ya vile mnavyostaili kwa hiki mlichonizushia leo ….mungu ni wetu sote na hasikilizi amri za binadamu so atakaponihitaji ataniita kwa mapenzi yake but si nyie east african vibes mnaoweza kuniua wala yeyote yule chini ya hili jua …

kama nyie hamuioni thamani yangu hilo ni juu yenu kwani huku niliko mimi ni kama lulu na maisha yanaendelea tena kwa kiwango cha juu kabisa ..hii si mara ya kwanza kunizushia kifo na mambo mengine ya ajabu ajabu ila all in all mi nipo na bado mtaniona sana nikiendelea kuwepo ….im total dissapointed kwakweli …mungu awape stahiki yenu ..THANKS SANA EATV 13/12/2016

3 comments:

  1. Aisee! Binadamu bana sijui wakoje.mungu azidi kukupa uhai Mr nice wanaokuzushia kifo basi watatangulia wao

    ReplyDelete
  2. Aisee! Binadamu hawa sijui vipi! Daah mungu azidi kukupa maisha marefu Na hawa wanaokuzushia kifo basi watatangulia wao.pole sana nice mungu ndiye anaepanga kifo chako Na sio mwanadamu

    ReplyDelete
  3. Aisee! Binadamu bana sijui wakoje.mungu azidi kukupa uhai Mr nice wanaokuzushia kifo basi watatangulia wao

    ReplyDelete

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.