Habari za Punde

MTIHANI WA KWANZA TPBC NI LEO, CHEKA ATAPANDA ULINGONI AU HAPANDI?

KWA mara ya kwanza TPBC leo kinatarajiwa kutoa msimamo wa kutojaribiwa na wanachama wake Kwa kuamua kuhusu suala la bondia Cheka kutangaza kutopanda ULINGONI kupambana na Dullah Mbabe jioni ya leo.

Kwa mujibu wa Ndg.Mohamed Kiganja Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo (BMT) ,Baraza ambalo ndio msimamiaji mkuu wa masuala ya Michezo Tanzaniac (Bara) aliitambulisha Tanzania Professional Boxing Commission TPBC kama ndiye msimamizi pekee aliyesajiriwa Kisheria kusimamia  Masuala yanayohusu Mchezo wa Ngumi za Kulipwa hapa Tanzania.

Ikumbukwe kuwa uhalali huu ambao unapewa chagizo mbalimbali za kupingwa na baadhi za wadau muhimu unakifanya TPBC kuwa ni chombo PEKEE kinachosimamia maslahi mapana ya ngumi za kulipa hapa nchini.

Uhalali huu wa kisheria kwa TPBC unatazamiwa uende na mfumo mzuri wa kiuongozi na kiutendaji ndani ya TPBC yenyewe ,Uhalali huu unategemewa kuwa usiruhu migongano wa kimaslahi kati ya TPBC ua wahusika wa TPBC na wadau mbalimbali wanaotambuliwa kama ni muhimu katika ngumi za kulipwa.

Uhalali wa TPBC na uwezo wake wa kusimamia maswala mazima ya Ngumi za kulipwa unajaribiwa leo katika mgogoro wa ama kufanyika au kutokufanyika kwa pambano la ngumi kati ya Bondia Francis Cheka na Abdallah Pazi (Dulla Mbabe).

Mtihani wa uhalali wa TPBC na kutosha kwake kisheria kuwa kama msimamiaji mkuu ni kwa TPBC kuonyesha uwezo wake wa kiutendaji na wa kisheria kwa kuhakikisha kuwa maafikiano yaliyofikiwa kati ya pande Tatu zinazohusika na pambano (Upande wa Bondia Francis Cheka ,Abdallah Pazi na Promoter Kaike) unatekelezwa kikamilifu.TPBC inatakiwa itoe suluhisho kwa ghalama zilizoingiwa na waandaaji wa pambano na mabondia zinafidiwa vipi?

Kabla ya pambano hili ama pambano lolote linguine TPBC inatakiwa ioanishe mambo ya msingi yanayotakiwa yawe kwenye mkataba wa Pambano la Ngumi ,TPBC inatakiwa iweke wazi kuwa ni nani anayeweza kuingia mkataba wa Pambano la Ngumi na ni utaratibu gani unaotakiwa kufwata katika kutekeleza malipo ya pambano husika,Hapa nina maanisha kuwa TPBC haitakiwi itengeneza mkataba bali inatakiwa iweke misingi muhimu ya kuufanya mkataba husika kuwa halali kwa tafsiri ya macho ya TPBC.

Kama Pambano halitaweza kufanyika ,TPBC itachukuwa hatua gani ya kutoa adhabu kwa wahusika waliovunja makubaliano hayo ,adhabu tunayoiangalia hapa ni ile ambayo itaweza kufidia ghalama za maandalizi ya Bondia/Mabondia husika ,ghalama za maandalizi ya pambano kutoka kwa Muuandaaji (Promoter) na ghalama na usumbufu walioupata wadau na mashabiki mbali mbali waliokuwa wamepanga kuudhuria pambano hilo ,lakini pia TPBC inaweka miongozo gani itakayosaidia kuondoa ubabaishaji wa namna hii kwenye mchezo wa Ngumi ili kuufanya mchezo huu kuwa sehemu salama kwa Mabondia na salama kwa wanaowekeza pesa zao pia!

Nina mashaka kama ni kweli TPBC ina uelewa sahihi wa ukubwa iliotwisha kisheria katika swala zima la Kusimamia Ngumi za kulipwa hapa Tanzania ,nina mashaka kama TPBC itakuwa na kanuni na Tratibu zinazoeleweka wazi kuhusiana na utekelezaji wa maswala mbali mbali yanayohusu Ngumi za kulipwa hapa Tanzania ,nina mashaka pia kama TPBC wanaweza kuwa na tafsiri sahihi ya utambuzi wa wahusika wakuu kwenye Maswala ya Ngumi za Kulipwa nikiwa na maana kwa Tafsiri ya TPBC inatambuaje kazi na muainisho wa kazi za Bondia ,Maneja wa Bondi ,Kocha wa Bondia ,Promoter wa Mchezo wa Ngumi…Nina wasiwasi kama TPBC ina utaratibu mzuri wa usajiri au utambuzi wa wadau mbali mbali wanaohusika na maswala haya ya ngumi za kulipwa wakiwemo MAbondia ,MApromoter ,MAkocha ,Waamuzi  ,MAdaktari na wadau wengine muhimu katika kufanikisha kufanyika kwa pambano lolote husika na kulinda maslahi ya kila mmoja katika watendaji hao.

TPBC isiwe ni chombo tu kinacho sanction (Kutoa ruhusa) ya mapambano na kuhakikisha ada mbalimbali zimelipwa bali kiwe ni chombo kinachosimamia kiujumla mazingira mazima ya mchezo husika na kuweka taratibu nzuri zitakazowezesha ustawi wa mchezo husika.

TPBC inatakiwa itambuwe ukubwa wa majukumu yake na yenyewe inatakiwa kuepuka kuwa sehemu yaTatizo/Matatizo ya kudumaza Ngumi za kulipwa hapa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.