Habari za Punde

NEC YAENDELEA NA MAANDALIZI YA UCHAGUZI MDOGO KATIKA JIMBO LA DIMANI MJINI ZANZIBAR

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Mstaafu Damiani Lubuva akiongoza kikao cha Wajumbe wa Tume na Sekretarieti kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani mjini Zanzibar leo Desemba 14, 2016 . Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan.
Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe.Jaji Mstaafu Mary Longway akizungumza jambo wakati wa kikao cha Wajumbe na Sekretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo Desemba 14, 2016 mjini Zanzibar. 
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Hamid M. Hamid (kushoto) akizungumza jambo wakati wa kikao cha Wajumbe na Sekretarieti ya Tume mjini Zanzibar leo. Katikati ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu Damian Lubuva na Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan (kulia).

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.