Habari za Punde

NEC YAKUTANA NA UGENI KUTOKA CHAMA CHA BODI ZAUCHAGUZI DUNIANI

Mkuu wa Sehemu ya Kanzidata ya Daftari na Mifumo ya Kijiografia wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Adolf Kinyero (kulia) akimuonesha Mtaalamu wa Uchaguzi kutoka Chama cha Bodi za Uchaguzi Duniani (AWEB) Park jae Sung (katikati) na Mtafiti wa Chama hicho, Moon Jueun, jinsi BVR inavyofanya kazi.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mipango na Operesheni kutoka Chama cha Bodi za Uchaguzi Duniani (AWEB), Lee Ju-Hwan (kulia) akieleza jambo kwa baadhi wajumbe wa Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) baada ya kutembelea tume hiyo jijini Dar es Salaam. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Mkurugenzi wa Manunuzi, Ugavi na Lojistiki wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Elied Njaila akisisitiza jambo kwa ugeni kutoka Chama cha Bodi za Uchaguzi Duniani (AWEB) (haupo pichani) ambao umetembelea Tume hiyo jijini Da es Salaam.
Mtaalamu wa Uchaguzi kutoka Chama cha Bodi za Uchaguzi Duniani (AWEB) Park jae Sung (aliyeshika mashine ya kusajili wapiga kura) akieleza utendaji kazi wa mashine hiyo kwa baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) (kulia).
Mkuu wa Sehemu ya Kanzidata ya Daftari na Mifumo ya Kijiografia wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Adolf Kinyero (kulia) akitoa maelezo kwa wajumbe kutoka Chama cha Bodi za Uchaguzi Duniani (AWEB) waliotembelea Bohari Kuu ya Serikali kujifunza mambo mbalimbali kutoka NEC.
Afisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Noah Kasekwa (kulia) akimpiga picha Mkurugenzi wa Kitengo cha Mipango na Operesheni wa Chama cha Bodi za Uchaguzi Duniani (AWEB), Lee Ju-Hwan kwa kutumia BVR kuonesha jinsi inavyofanya kazi. 
Mtaalamu wa Uchaguzi kutoka Chama cha Bodi za Uchaguzi Duniani (AWEB) Park jae Sung (katikati) akiwaeleza baadhi ya Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhusu kifaa kinachotumia Teknolojia ya Kuandikisha wapiga Kura. 
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Kailima Ramadhani (wa tatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni kutoka Chama cha Bodi za Uchaguzi Duniani (AWEB).Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mipango na Operesheni, Lee Ju-Hwan, Mtafiti, Moon Jueun na Mtaalamu wa Uchaguzi, Park jae Sung.Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Daftari la Wapiga Kura, Mhandisi Manyiri Isack na Mkuu wa Sehemu ya Kanzidata ya Daftari na Mifumo ya Kijiografia, Adolf Kinyero. 
Baadhi ya Watendaji kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wageni wao kutoka Chama cha Bodi za Uchaguzi Duniani (AWEB) kwenye ofisi za Tume hiyo zilizoko Bohari Kuu ya Serikali jijini Dar es Salaam, baada ya wageni hao kufika kwenye ofisi hizo kujifunza mambo mbalimbali kutoka NEC.
Mashine inayotumika kuandikisha Wapiga kura inayotumia Teknolojia ya Kisasa ambayo Tume ya Taifa ya Uchaguzi imejifunza jinsi mashine hiyo inavyofanya kazi. Picha na Hussein Makame, NEC
*********************************
Christina Njovu, NEC
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imepokea ujumbe Taasisi ya Tume za Uchaguzi Duniani (AWEB) uliokuja kujifunza na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya uendeshaji Uchaguzi.

Ujumbe huo umekuja kujifunza kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) juu ya masuala mbalimbali ya uendeshaji Uchaguzi nchini ikiwemo matumizi ya vifaa vya kuandikishia wapiga kura. 

Mkurugenzi wa Mipango na Oparesheni Bw. Lee Ju-Hwan alisema kuwa yeye na ujumbe wake wamekuja kubadilishana uzoefu katika technolojia ya Kuandikisha Wapiga Kura. 

Ujumbe huo umekutana na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Bw. Kailima Ramadhani na kufanya mazungumzo naye ofisini kwake baada ya kukutana na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya tume hiyo kutembelea ofisi mbalimbali za Tume hiyo na kujifunza. 

Wakiwa katika kikao na baadhi ya Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ujumbe huo wa watu watatu ulijifunza namna mashine ya Biometric Voter Registration (BVR) inavyofanya kazi na jinsi NEC ilivyoweza kuandikisha Wapiga Kura wengi kwa kutumia mashine technolojia hiyo na changamoto zake. 
Aidha ujumbe huo umekuja na aina mpya ya technologia ambayo inauwezo wa kuandikisha Wapiga Kura, kutuma taarifa za Wapiga katika kanzidata kutoka katika kituo cha kujiandikishia na kuhakiki Wapiga Kura siku ya Uchaguzi . 

Mashine hiyo ambayo ni ndogo ukilinganisha na ile BVR ina uwezo wa kutumiwa na mtu mmoja ambaye ataweza kumuandikisha Mpiga Kura katika hatua zote hadi kupata kitambulisho cha mpiga Kura na inabebeka kirahisi. 

Ujumbe huo umeongozwa na Mkurugenzi wa Mipango na Operesheni Lee Ju-Hwan, Mtafiti Moon Jueun na Mtaalamu wa Uchaguzi Park Jae Sumg.

Technologia hiyo mpya inaweza kurahisisha utendaji kazi katika masuala ya uandikishaji wapiga Kura, kuhakiki wapiga kura na kutuma taarifa katika kanzi dara.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.