Habari za Punde

NICOL KUENDELEZA UWEKEZAJI WA HISA NCHINI.

Mwenyekiti wa kampuni ya Uwekezaji wa  Taifa (NICOl) Bw. Gideon Kaunda  kulia akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es salaam mara baada ya kupata uongozi mpya wa kampuni hiyo ulioteuliwa rasmi hivi karibuni na bodi ya NICOL kushoto ni Mtendaji Mkuu Bw. Adam Wamunza. Picha Na Ally Daud-Maelezo
***********************************************
Na Ally Daud-MAELEZO
Kampuni inayojihusisha na uwekezaji nchini (NICOL) imejidhatiti  kuendeleza  uwekezaji wa hisa nchini ili kukuza uwekezaji wa ndani na kuleta ushindani kwa wawekezaji ndani na nje.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa kampuni ya Uwekezaji wa  Taifa (NICOl) Bw. Gideon Kaunda wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam.

 “Sasa tunahitaji kuendeleza uwekezaji wa ndani katika hisa na hivi karibuni tumenunua hisa ili kukuza uwekezaji na kuleta ushindani kwa wawekezaji wa nje katika soko huria” alisema Bw. Kaunda.

Aidha Bw. Kaunda amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanapata wawekezaji wa ndani ili kukuza uchumi wa nchi pamoja na kuweza kuleta ushindani .

 Mbali na hayo Bw. Kaunda amesema kuwa wanataraijia kuwekeza kwenye sekta zote za uchumi kama mazao ya biashara ikiwamo korosho,gesi, mafuta  pamoja na madini ili kuweza kutangaza bidhaa za Tanzania kwenye soko la nje.

Aidha Bw. Kaunda aliwataka wawekezaji wote wa ndani na wa nje kushirikiana na NICOL katika shughuli za uwekezaji hasa wa mazao ya biashara ili kuipeleka  Tanzania katika soko la kimataifa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.