Habari za Punde

RAUNDI YA TATU MICHUANO YA KOMBE LA AZAM 2016 KUENDELEA KESHO

Raundi ya Tatu ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam 2016 (Azam Sports Federation Cup 2016) inatarajiwa kuendelea kesho Desemba 3, 2016 kwa michezo minne itakayokutanisha timu nane zilizofanya vema raundi ya kwanza na pili.
Michezo ya kesho ambayo itakuwa mubashara (live), kupitia chaneli mbalimbali za Kituo cha Televisheni cha Azam ‘Azam Tv’ itakuwa ni kati ya Mtwivila ya Iringa na Jangwani ya Rukwa mchezo unaotarajiwa kufanyika mkoani Iringa wakati Stand ya Bagamoyo itacheza na Mbuga ya Mtwara kwenye Uwanja wa Mabatini, ulioko Mlandizi mkoani Pwani.

Stand Misuna ya Singida inatarajiwa kuwa wenyeji wa Kabela City ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida wakati Mulusagamba ya Kagera na Baruti ya mkoani Mara zitachuana kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera katika mfululizo wa mechi hizo.

Mechi hizo zitatoa timu nne bora kutoka mabingwa wa Mkoa na hivyo kuungana na timu 24 za Ligi Daraja la Pili kwa michezo ya hatua ya raundi ya nne na tano kutafuta timu nane bora zitakazosonga mbele kukutana na timu za Daraja la Kwanza.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.