Habari za Punde

RC MAKONDA AANZA UJENZI WA MAHAKAMA 20 JIJINI DAR

Mkuu wa Mkoa Wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujenzi wa Mahakama utapunguza mzigo mkubwa kwa Serikali na itasaidi wakazi Nje ya Dar es salaam na Ndani katika kupata Haki Zao za kisheria kwa haraka leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Harrison Mwakyembe
**************************************************
Na Anthony Johny,Dar 
MKUU wa Mkoa Wa Dar es salaam Paul Makonda ameahidi kuanza Ujenzi wa Mahakama 20 za Mwanzo katika Mkoa wa Dar es salaam ili kupunguza msongamano wa mahabusu katika vituo vya polisi na Magereza.

Hayo ameyasema leo Makonda wakati alipotembelewa na Waziri wa Katiba na Sheria, Harrison Mwakyembe, ofisini kwake, amesema ujenzi huo wa Mahakama utapunguza mzigo kwa Serikali na itasaidia wakazi walio nje kidogo jiji la Dar es salaam kuweza kupata haki kwa wakati.

Makonda alitoa wito kwa badhi ya Wadau mbalimbali kujitokeza ili kusaidia ujenzi wa Mahakama hizo, Amesema mtu yeyote atakaye kwenda kinyume na sheria hatakama alisaidia kujenga Mahakama, sheria itafata mkondo wake.

Nae Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Harrison Mwakyembe amempongeza Makonda kwa kutafuta vijana wanasheria na kuwapeleka katika kila Wilaya katika jiji la Dar es salaam ilikuweza kuwaidia wananchi kuwanyonge kupata haki katika masuala ya kisheria.

" Sisi kama Wizara tunampongeza Mkuu wa Mkoa kwa kuwatafuta vijana mbambali wanasheria na kuwapeleka katika kila Wilaya ilikuweza kuwasaidia wananchi hawa kupata msaada wa kisheria ilikupunguza uonevu kwa baadhi ya watu".amesema Mwakyembe.

Amesema katika ujenzi huo wa Mahakama za mwanzo kutawasaidia wakazi mbalimbali wa jiji la Dar es salaam kuwa na uhakika wa kupata haki kwa wakati mwafaka na kupunguza baadhi ya migogoro katika jamii na serikali..
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari juu ya amempongeza Makonda kwa kutafuta vijana wanasheria na kuwapeleka katika kila Wilaya ya Dar es salaam ilikuweza kuwaidia wananchi wanyonge katika masuala ya kisheria, leo jijini Dar es Salaam. Kukia ni Mkuu wa Mkoa Wa Dar es salaam Paul Makonda. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Harrison Mwakyembe akisanikitambu cha wageni katika ofisi ya mkuu wa mkoa leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda Katibu Mkuu wa Sheria na Katiba, Profesa Sifuni Mchome, Naibu Katibu Mkuu wa Sheria na Katika, Amon Mpanju

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.