Habari za Punde

SERIKALI YA TANZANIA NA MAURITIUS KUENDELEZA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA SANAA NA UTAMADUNI

 Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa,na Michezo Mhe. Anastazia Wambura(wa pili kulia) akizungumza na Ujumbe  wa Serikali ya Mauritius pamoja na  baadhi ya viongozi wa Wizara  leo Jijini Dar es Salaam  alipokutana na Waziri wa Sanaa na Utamaduni Mhe. Santaram Baboo (wa kwanza kulia) kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika sekta ya Sanaa na Utamaduni.Wa tatu kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel.
 Viongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo  wakiwa katika mazungumzo na Uongozi wa Mauritius kuhusu kuimarisha sekta ya Sanaa na Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Mauritius Mhe.Santaram Baboo (wa kwanza Kulia) akizumgumza na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo wakati wa majidiliano ya  kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili  katika Sekta ya Sanaa na Utamaduni yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Anastazia Wambura.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel(aliyesimama) akiongea jambo wakati wa mazungumzo  kati ya Wizara yake na Serikali ya Mauritius katika  Sekta ya Sanaa na Utamaduni.
 Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa,na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Mauritius Mhe.Santaram Baboo baada ya mazungumzo baina yao kuhusu ushirikiano katika Sekta ya Sanaa na Utamaduni yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa,na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara yake na viongozi wa Serikali ya Mauritius baada ya mazungumzo kuhusu ushirikiano katika Sekta ya Sanaa na Utamaduni yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa,na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara yake na viongozi wa Serikali ya Mauritius baada ya mazungumzo kuhusu ushirikiano katika Sekta ya Sanaa na Utamaduni yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.