Habari za Punde

SERIKALI YAVUKA LENGO ONGEZEKO LA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA KIFEDHA KUPITIA SIMU ZA MIKONONI.


Idadi ya Watu wazima wanaotumia huduma za kifedha kupitia simu za mkononi imeongezeka kutoka asilimia 61 ya mwaka 2014 hadi kufikia asilimia 80 ya mwaka 2016.

Akiongea wakati akiwasilisha matokeo ya tafiti ya matumizi ya huduma rasmi za kifedha nchini Meneja Mradi wa Sauti za Wananchi kutoka asasi ya TWAWEZA Nellie Njovu alisema kuwa ongezeko hilo limevuka lengo la serikali waliojiwekea kufikisha huduma za kifedha kwa asilimia 50 ya watanzania ifikapo 2016.

Aidha Bi. Nellie alisema kuwa asilimia 80 ya watumiaji wa huduma za kifedha kupitia mitandao ya simu wamesema wanaridhishwa na huduma zinazotolewa na ni mtumiaji mmoja kati ya kumi anayesema haridhishwi na huduma hizo.

Matokeo haya yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutpka kwa wahojiwa 1800 kutoka maeneo mbalimbali Nchini kati ya terehe 14 hadi 26 septemba 2016.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.