Habari za Punde

SHIME AKABIDHIWA MIKOBA YA MALALE HAMSINI KUINOA JKT RUVU

Na Zainab Nyamka, Dar
TIMU ya JKT Ruvu imefanikiwa kunasa saini ya kocha wa timu ya Vijana Chini ya miaka 17 Serengeti Boys Bakari Shime na kumpatia kandarasi ya miaka miwili ili kuweza kukinoa kikosi hicho cha maafande.

Shime amechukua nafasi ya Mzanzibar Malale Hamsini aliyekuwa anakinoa kikosi hicho raundi ya kwanza lakini akishindwa kuipatia matokeo timu hiyo.

Mkurugenzi wa Ufundi wa JKT Ruvu Kocha mwandamizi Abdalla Kibadeni amesema kuwa uamuzi huo umekuja baada ya uongozi wa juu kuona kuwa Kocha Malale Hamsini ameshindwa kuipatia matokeo timu yake na kama raundi ya pili ikiendelea hivyo basi inaweza ikashuka daraja.

Kibadeni amesema kuwa, kwa sasa Shime amepewa nafasi ya kuangalia wachezaji wa timu ya vijana kuangalia kama anaweza kuwatumia kwani hawana malengo ya kufanya usajili wowote kwa wachezaji kutoka timu nyingine.

Shime ameweza kufanikiwa kufanya vizuri na timu ya vijana ya Serengeti Boys kwahiyo wana imani naye kuweza kuisaidia timu ya JKT Ruvu katika duru la pili ambapo kwa sasa ipo nafasi ya tatu kutoka Chini.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.