Habari za Punde

SIMBA WAENDELEA KUJICHIMBIA KILELENI WAICHAPA JKT RUVU BAO 1-0

Simba SC leo tena wameendelea kujikusanyia pointi tatu na bao moja katika Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuwechezesha kwata maafande wa JKT Ruvu na kuibuka na bao 1-0 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.


Ligi hiyo imeendelea leo kwa michezo sita kupigwa huku Simba wakiwa wenyeji walipata bao lakatika dakika ya 49 kipindi cha kwanza lililofungwa na Muzamir Yassin.

Kwa ushindi huo Simba wanaendelea kubaki kileleni wakiongoza Ligi hiyo wakiwa na jumla ya Pointi 42 wakiwaacha watani zao wa Jadi Yanga kwa tofauti ya Pointi 4.
MATOKEO MENGINE YA MECHI ZA LEO:
Azam Fc 1- Majimaji 1
Kagera Sugar 1 - Stand United 0
Ndanda Fc 0 - Mtibwa Sugar 2
Simba SC 1 - JKT Ruvu 0
Mbeya City 0 - Toto African 0


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.