Habari za Punde

SIMBA WACHUKUA BANDO LAO LA WIKI KWA WATANI ZAO WAREJEA KILELENI, AZAM YAVUTWA SHATI NA AFRICAN LYON

TIMU ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam, leo imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ndanda Fc katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa jioni hii kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Katika mchezo huo bao la kwanza lilifungwa na Muzamir Yassin, katika dakika ya 63, na bao la pili likifungwa na Mohamed Ibrahim

Katika matokeo mengine ya mechi za leo za Ligi Kuu Bara, Azam Fc wametoshana nguvu na African Lyon 0-0 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Na huko jijini Mbeya, Tanzania Prisons wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Majimaji, katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini humo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.