Habari za Punde

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UCHAGUZI WA VIONGOZI WA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA

Katibu wa Baraza la Vyama vya Siasa anatumia fursa hii kuutangazia umma na wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa kuwa, kutakuwa na uchaguzi wa viongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa utakaofanyika tarehe 19 Disemba, 2016 Dar-es salaam.

Uchaguzi wa viongozi wa Baraza unafanyika kwa mujibu wa Kanuni za Baraza la Vyama vya Siasa. 

Uchaguzi utakaofanyika ni wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, ambao muda wao wa uongozi unaisha tarehe 19 Disemba, 2016. 

Fomu za kugombea zitatolewa kuanzia tarehe 07 Disemba, 2016 saa tatu asubuhi katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa hapa Dar-es salaam na zinatakiwa kurejeshwa siyo zaidi ya tarehe 12 Disemba, 2016 saa tisa na nusu mchana katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa hapa Dar-es salaam. 

Aidha, fomu zinapatikana pia katika tovuti ya ofisi www.orpp.go.tz

Hivyo, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inawaomba wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa wenye nia ya kugombea nafasi hizo, kuchukua fomu, kuzijaza kikamilifu na kuzirudisha kwa wakati. 

Kanuni za Baraza la Vyama vya Siasa zinakataza mjumbe wa Baraza kugombea nafasi zaidi ya moja. 

Sisty L. Nyahoza
Kny: KATIBU WA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA
06 Disemba, 2016

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.